Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Mwinyi Amejumuika na Wananchi Katika Sala ya Ijumaa Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Unguja

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akisalimiana na Balozi Mdogo wa Oman hapa Zanzibar Mhe.Said Salim Al Sinawi pamoja na Viongozi wengine wakati alipowasili katika Masjid Jamiuu Zinjibar Mkoa wa Mjini Magharibi  leo kushiriki katika Swala ya Ijumaa.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (wa tatu kulia) pamoja na Waumini wakiitikia Dua ilikisomwa na  Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi(katikati)  baada ya Ibada ya   Swala ya Ijumaa katika  Masjid Jamiuu Zinjibar Mazizini  Mkoa wa Mjini Magharibi.
Waumini wa Dini ya Kiislamu waliohudhuria Ibada ya Swala ya Ijumaa leo, Masjid Jamiu Zinjibar,Mkoa wa Mjini Magharibi wakiitikia Dua Iliyoombwa baada ya  ibada hiyo, iliyowajumuisha  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi na Viongozi mbali mbali.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akiteta na Mkurugenzi wa Mkuu wa Kituo cha Ahmed Al Faatih  cha Kiislamu -Bahrain Bw.Nawaf Rasshid Al Rashid (katikati) baada ya Ibada ya   Swala ya Ijumaa katika  Masjid Jamiuu Zinjibar Mazizini  Mkoa wa Mjini Magharibi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akisalimiana na Sheikh Salum Mardhia baada ya kumalizika kwa ibada ya Sala ya Ijumaa Leo katika masjid Jamiuu Zinjibar Mazizini  Mkoa wa Mjini Magharibi.
[Picha na Ikulu] 29/09/2023.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.