Habari za Punde

Zimamoto yaigaragaza Ngome Ligi Kuu ya Zanzibar. "PBZ Premier League" Zimamoto Imeshinda Mchezo huo kwa Bao 5-0

Mchezaji wa Timu ya KZU na wa Timu ya Ngome wakiwania mpira katika mchezo wao wa ufunguzi wa Ligi Kuu ya Zanzibar "PBZ Premier League " mchezo uliyofanyika katika Uwanja wa Mao Zedung .Timu ya KZU imetoka kivua mbele kwa ushindi wa bao 5-0 dhidi ya Timu ya Ngome.

NA MWAJUMA JUMA

MAAFANDE wa timu ya soka ya Kikosi Cha Zimamoto na Uokozi (KZU), imetoka kidedea mbele Ngome kwa kuifunga mabao 5-0 katika mchezo wa ligi kuu uliochezwa Mao Zedong A.

Mchezo huo ambao ulihudhuriwa na mashabiki kiasi ulichezwa majira ya saa 10 za jioni ambapo hadi mapumziko  timu ya Zimamoto ilikuwa ikiongoza kwa mabao 3-0.

Katika mchezo huo Zimamoto mabao yake matatu yalifungwa na Ibrahim Hamad Hilika katika dakika za 29, 43 na 89 na mawili yalifungwa na Hussein Mwinyi Mohammed dakika ya 45 na Seif Mmadi Khamis dakika ya 55.

Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea tena kesho Alhamis kwa kuchezwa michezo miwili, ambapo 
Kundemba itacheza na Jamhuri uwanja wa Mao Zedong A na  Hard Rock itapambana na Mafunzo  katika dimba la Finya kisiwani Pemba.

Kikosi cha Timun ya KZU kilichoaza katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya Zanzibar umchezo uliofanyika katika Uwanja wa Mao Zedung na kutowa Kipigo cha Bao 5-0 dhidi ya Timu ya Ngome.
Kikosi cha Timu ya Ngome kilichokubali Kipigo cha bao 5-0 dhidi ya Timu ya KZU katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya Zanzibar "PBZ Premier League "uliofanyika katika Uwanja wa Mao Zedung 
No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.