Habari za Punde

BUNGE LA TANZANIA NA SHIRIKA LA UNDP WASAINI MKATABA WA DOLA MILION 2.5

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa UNDP Ndg. Sergio Valdini wakisaini andiko la Mradi wa awamu ya tatu la kuwajengea uwezo Wabunge na Watumishi wa Bunge lenye thamani ya Dola za Kimarekani 2,596,001.00 katika Ofisi Ndogo za Bunge zilizopo Jijini Dar es Salaam. Pembeni ni Katibu wa Bunge Bi. Nenelwa Mwihambi akishuhudia tukio hilo.

Bunge la Tanzania na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) wamesaini Andiko la Mradi wa Awamu ya Tatu wa Kuwajengea uwezo Waheshimwa Wabunge na Watumishi wa Bunge (LSP III) wenye thamani ya Dola za Kimarekani 2,596,001.00. Aidha, Mradi huo utahudumia pia Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

Andiko hilo limesainiwa leo tarehe 11 Oktoba, 2023 katika Ofisi Ndogo za Bunge zilizopo Jijini Dar es Salaam ambapo Utekelezaji wa Mradi huo utaanza Mwezi Oktoba 2023 hadi Novemba 2027.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson akibadilishana hati na Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa UNDP Ndg. Sergio Valdini mara baaada ya kusaini andiko la Mradi wa awamu ya tatu la kuwajengea uwezo Wabunge na Watumishi wa Bunge lenye thamani ya Dola za Kimarekani 2,596,001.00  katika Ofisi Ndogo za Bunge zilizopo Jijini Dar es Salaam.  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.