Habari za Punde

DC Kaskazini A azindua mradi wa usimamizi shirikishi wa uvuvi katika Hifadhi ya TUMCA Mkuu wa Wilaya Kaskazini A Unguja Mhe Sadifa Juma tarehe 16/10/2023, amezindua mradi wa usimamizi shirikishi wa uvuvi katika Hifadhi ya TUMCA unaofadhiliwa na shirika la Blue Venture (BV). Mradi huo ni wa mwaka mmoja utakaotekelezwa na JDF kwa mashirikiano na usimamizi wa Hifadhi ya TUMCA.

Mradi huu unalenga kuimarisha uendeshaji wa usimamizi wa rasilmali katika Hifadhi ya TUMCA. Hafla hii fupi ya uzinduzi, pia ilijadili namna mradi utakavoweza kuimarisha uhifadhi na kuongeza uwelewa juu ya matumizi bora na endelevu ya rasilimali za bahari ndani ya hifadhi ya TUMCA na namna sahihi ya kutatua migogoro ya kiuvuvi katika jamii hizo ili kufikia malengo ya uvuvi na utalii endelevu kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.