Habari za Punde

Rais Samia Suluhu Hassan afungua Daraja la Msingi lililopo Mkalama Mkoani Singida

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa pamoja na viongozi wengine wakati akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Daraja la Msingi lililopo Mkalama Mkoani Singida tarehe 16 Oktoba, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa wakati wakivuta kitambaa kuashiria ufunguzi wa Daraja la Msingi lililopo Wilayani Mkalama Mkoani Singida tarehe 16 Oktoba, 2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa wakati akikagua Daraja la Msingi lililopo Mkalama Mkoani Singida tarehe 16 Oktoba, 2023

Viongozi mbalimbali pamoja na Wananchi waliohudhuria tukio la ufunguzi wa Daraja la Msingi lililopo Mkalama Mkoani Singida tarehe 16 Oktoba, 2023

Taswira ya Daraja la Msingi lenye urefu wa Mita 100, lililopo katika Kijiji cha Msingi, Mkalama Mkoani Singida. Daraja hilo limezinduliwa Rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan tarehe 16 Oktoba, 2023

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.