Habari za Punde

Wananchi Watakiwa Kujiunga na Bima ya Taifa ya Afya Kabla ya kuaza Kuungua

Na Lucas Raphael,Tabora

Wananchi wameshauriwa kujiunga na mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF)kabla ya kuanza kuungua ili kurahisisha mchato wa kupata matibabu ya haraka yanatolewa na mfuko huo nchini .

Akizumgumza na waandishi wa habari leo kwenye ukumbi wa mikutano wa mkuu wa mkoa wa Tabora Meneja wa mfuko wa Taifa wa bima ya afya mkoa humo ,Salum Adam alipokuwa akitolea ufafanuzi wa maswala mbalimbali yanayohusu mfuko huo  .

Alisema kwamba wananchi wanapaswa kujiunga na mfuko huo kabla ya kupata maradhi ili iwe rahisi kuweza kupata huduma ya matibabu yanayootolewa katika hospitali mbalimbali nchini .

“Ipo tabia ya watu kujiunga na mfuko wa Taifa wa bima ya afya baada ya kuungua jambo ambalo sio nzuri na hali hiyo inasababisha kukosa matibabu kwenye hospitali zinazotoa huduma ya mfuko wa Taifa bima ya Afya“alisema Adam.

Alisema kwamba iwapo mfuko huo ungekuwa unatoa huduma za aina hiyo utafilisika na utashindwa kutoa huduma kama ilivyokusudiwa na malengo ya serikali ya kutoa huduma za afya kwa wananchi wake .

Akizungumza changamoto ya kuchelewa kwa kadi za bima Meneja huyo aliendelea kusema kwamba  mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF) mkoani hauna changamoto ya ucheweleshaji wa vitambulisho isipokuwa kuna changamoto ya kimazingira na mfumo uwasilishaji wa kadi kwa wanachama kupitia halmashuari zao .

Alisema kwamba mchakato wa kuwafikishia kadi wanachama ambao wengi ni watumishi wa serikali umekuwa ukifanyika kupitia Halmashauri na hivyo muda wa kupata kadi unatengemea umbali wa mwanachama husika hasa joghafia ya halmashauri yake .

“mtumishi akijaza fomu ya bima kwanza anaipeleka halmashauri kisha halmashauri inaipeleka fomu ofisi za NHIF na baada ya mchakato wa kadi  NHIF hurudisha tena halmashauri mchakato ambao unaweza kuchelewa kadi   kufika kwa mwanachama aliye mazingira ya mbali”alisema Adam.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.