Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum, ambaye anaongoza Ujumbe wa Tanzania katika Mikutano ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), kwa niaba ya Waziri wa Fedha wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Uendeshaji wa Benki ya Dunia (World Bank Managing Director for Operations) Bi. Anna Bjerde, kando ya Mikutano ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), inayofanyika Jijini Marrakech, nchini Morocco, ambapo wamejadiliana kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo maandalizi ya Mkutano wa Kimataifa wa Tathimini ya Muda wa Kati wa Mzunguko wa 20 wa Benki ya Dunia (IDA20 Medium Term Review) utakaofanyika Zanzibar kuanzia tarehe 6 hadi 8 Desemba, 2023, ukishirikisha wajumbe zaidi ya 250 kutoka mataifa takribani 100 duniani.
MKURUGENZI MOSHI ATOKWA MACHOZI, CCM NA CHADEMA WAKIMPA ZAWADI .
-
Mkurugenzi wa Halmashauriya Manispaa ya Moshi Mwajuma NAsombe akizungumza
wakati wa kikao cha mwisho cha Bajeti cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri
.
...
7 hours ago
No comments:
Post a Comment