Habari za Punde

Wizara ya Elimu kukutana na wadau wa Elimu majimboni






 Waziri wa elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Lela Muhamed Mussa amesema Wizara itahakikisha inakutana na wadau wa Elimu ndani ya Majimbo yote ya Zanzibar ili kuendelea kuimarisha sekta hiyo nchini.

Amesema hayo wakati wa Mkutano maalum wananchi wa Jimbo la Mwera katika uwanja wa Skuli ya Regeza Mwendo Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
Amesema ni kipao mbele cha serikali kuhakikisha kila mtoto anapata elimu.
Amesema ili kufikia vyema malengo hayo ya Serikali ni vyema Wizara kushuka Chini kwa Wananchi ili kuskiliza mawazo yao na kuweza kuitumia mitaala vyema kwa lengo la kuendeleza elimu nchini.
Aidha amesema Serekali imeiongezea bajeti Wizara ya Elimu ili kuhakikisha taifa linazalisha wasomi wazalendo.
Amesema ni jitihada za Serekali kuboresha miundombinu na mishahara kwa walimu ili watoto wapate elimu bora hivyo wazazi na jamii kwa ujumla kushirikiana katika jitihada hizo ili kufanikisha malengo hayo na kupelekea kukuza ufaulu wa daraja la awali .
Aidha Waziri Lela amewataka wenyeviti kuendelea kuwasisitiza wazazi,walezi na jamii kuhakikisha wanasimamia watoto wao ili wapate elimu kwanza.
Amesema Serekali kupitia Wizara ya Elimu itafanya mageuzi makubwa ya elimu na kuhakikisha watoto watakapo maliza masomo wanapata ujuzi maalum utakaompelekea mtoto kuweza kujitegemea mara baaada ya kumaliza masomo ya lazima.
Mapema mwakilishi wa jimbo hilo Mhe Mihayo Nhunga amesema suala la elimu ni suala linalohitaji mashirikiano ya kila mtu kwa namna yake ili kufikia malengo ya serikali hivyo ni vyema kila mmoja kuchukua hatua kwa upande wake ili kukuza ufaulu nchini.
Kwa upande wao Walimu Wakuu na wenyeviti wa
Kamati za skuli wamesema uchache wa walimu wa masomo ya sayansi ni changamo kubwa katika skuli nyingi zilizomo ndani ya jimbo hilo.
Aidha wamesema tatizo la uchakavu wa madarasa na wingi wa wanafunzi madarasani nalo bado linahitaji jitihada zaidi ili kufikia malengo ya serikali ya kuzalisha wataalamu wazalendo .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.