Habari za Punde

Wizara ya Habari na miaka mitatu ya Dk Mwinyi

 NA FAUZIA MUSSA     MAELEZO ZANZIBAR

 

Ama hakika mitatu inajieleza, katika kipindi kifupi tu cha uongozi wa  awamu hii ya nane mengi yamefanyika na kuonekana waziwazi.

 

Ni mafanikio tu ambayo yamewagusa wananchi kwa mtu mmoja mmoja na kwa makundi miongoni mwa wanufaika hao ni Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na sekta zake.

 

Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ni miongoni mwa Wizara zinazoendelea kufanya vizuri katika utendaji wake chini ya uongozi wa Serikali ya awamu ya nane inayoongozwa na kiongozi Jemedari na kipenzi cha Wengi Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

 

Wizara hii inayongozwa na Waziri kijana, Mwanamke mwenye umakini na umahiri katika utendaji wake nae ni Mhe. Tabia Maulid Mwita mwenye nia na dhana madhubuti ya kuwasimamisha na kuwaendeleza vijana katika nyanja mbali mbali za kiuchumi nchini.

 

Waziri huyo anapigana kwa kila hali kuunga mkono na kuhakikisha adhma ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi  ya kutoa ajira laki tatu kwa vijana inafikiwa.

 

Wizara ya Habari Zanzibar imegawika katika sekta kuu nne ambazo ni Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, katika miaka mitatu ya Uongozi wa Dkt. Mwinyi Sekta zote hizi zimefanikiwa katika mambo mbalimbali.

 

Tuangazie baadhi ya mafanikio yalitopatikana katika Wizara hii katika kipindi kifupi cha uongozi wa Dkt. Mwinyi.  

 

HABARI

Katika Sekta hii Wizara imefanikiwa kuleta mabadiliko mbali mbali kimuonekano na kiutendaji kwa ufanisi wa hali ya juu katika taasisi zote zinazohusiana na habari.

 

katika kipindi cha miaka mitatu ya Dkt. Mwinyi Wizara imefanikiwa kuanzisha nembo ya utambulisho wa Idara ya Habari Maelezo, kukamilisha mchakato wa kuwepo sheria  mpya ya habari inayoendana na wakati  ambayo muda si mrefu itapitishwa katika Baraza la Wawakilishi pamoja na kuisimamia na kukamilisha  Sera ya habari inayoendana na wakati tulionao na inayotekelezeka .

Aidha Wizara imefanikiwa kubadilisha muonekano wa Gazeti la Zanzibra leo na kulifanya kuwa na viwango na mvuto zaidi pamoja na kubadilisha bei ya kuuzia gazeti hilo kutoka 500-1000 na kufanikiwa kusambaza gazeti kutoka mikoa 11-31 ya Tanzania na kila Wilaya kwa baadhi ya Mikoa.

Kiujumla Tanzania nzima inafikiwa na taarifa kupitia Gazeti la Zanzibar leo katika kipindi hiki cha miaka mitatu ya Dkt. Mwinyi.

Hata hivyo ndani ya miaka mitatu Wizara imefanikiwa kubadilisha muonekano mzima wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) kwa kuboresha  vipindi na kuanzisha vipindi vyenye ubora na mvuto zaidi kwa watazamaji ambavyo vinatangazwa na Shirika hilo  pamoja na kutengeneza Studio tano  ndani ya jengo hilo kwa kipindi kifupi cha uongozi wake.

Aidha Rais wa Zanzibar amefanikiwa kuifikisha Wizara kukamilisha azma ya kuyawezesha mashirika kujiwezesha kibiashara na sasa Shirika la Magazeti na Wakala wa Serikali wa Uchapaji wameacha kabisa kupokea ruzuku kutoka Serikalini.

Hata hivyo, Wizara imefanikiwa kuliimarisha Shirika la Wakala wa uchapaji na kufanikiwa kununua mitambo mipya huku likiendelea na   kuchapa kazi za Serikali na binafsi kwa ufanisi Mkubwa na kuingiza kipato.

Vilevile  Wizara hiyo imevuka malengo kupitia  Tume ya Utangazaji ambapo imefanikiwa kuongeza mapato kutoka  milioni 150 hadi 310 kwa mwaka wa fedha uliopita.

Tume hii ina jukumu la kuvisimamia na kusajili vyombo mbalimbali vya habari vya binafsi pamoja na Serikali viliopo nchini.

Wizara imefanikiwa  kuongeza idadi ya wateja (Subscribe)  zaidi ya milioni moja na sasa  inaendelea  kukamilisha mpango wa uwekezaji unaokwenda kuisadia  kampuni ya kuunganisha na kusambaza  maudhui ZMUX kuwa na minara yao ya mawasilano na kuongeza ving’amuzi zaidi ya elfu tatu  kwa lengo la kuongeza  wateja wengi zaidi .

VIJANA

Kwa upande wa Vijana, kuna Sekta mbili ambazo zinasimamia maslahi ya vijana ikiwa ni pamoja na idara ya maendeleo ya Vijana na Baraza la Vijana ambalo lipo katika ngazi ya Shehia hadi Taifa.

Wizara imefanikiwa kujenga vituo vya maendeleo ya Vijana Unguja na Pemba, kwa upande wa pemba kituo cha maendeleo ya Vijana (YTC) kipo maeneo ya Weni Wete na Unguja kipo Bweleo Wilaya ya Magharibi ‘B’.

Vituo hivi vimekuwa vikitoa elimu ya ujasiriaali, ufundi pamoja na  kukuza Vipaji tofauti kwa  Vijana ili kuepusha vijana hao kujiunga na vigenge viovu na kuanza kujishughulisha na shughuli za ujasiriamali na kujiendeleza kiuchumi.

Vituo hivvyo vitawasaidia wanafunzi waliokosa  elimu ya msingi (basic education) kupata nafasi ya kuingia katika mfunzo kwa ghara nafuu na kutoka na ujuzi utakaowasaidia  kujiendeleza kiuchumi.

Wizara imefanikiwa Kuwapatia  miundombinu wezeshi vijana  wanaojishuhulisha na mradi wa kilimo cha pesheni Pagali Unguja ikiwemo mipira ya kusambazia maji, matangi ya kuhifadhia maji pamoja na nguzo za umeme kurahisiha upatikanaji wa maji hayo ili kuboresha na kuendeleza kilimo hicho, vijana hao wamefanikiwa kujiajiri na kuajiri wengine.

Aidha Wizara imefanya mazungumza na wadau mbalimbali wa mahoteli na mikahawa ili  kuwaunganisha vijana hao na wateja na  kuwapatia  soko la uhakika.

Katika miaka mitatu ya Dkt. Mwinyi Serikali imewekeza zaidi ya Shilingi Milioni 36 katika benki ya CRDB ili kuwasaidia Vijana kupata mikopo ili kujiendeleza kibiashara na kiubunifu.

UTAMADUNI

Sekta hii ni sekta inahusisha kazi zote za sanaa  na ina jukumu la kulinda na kuutetea utamaduni wa Mzanzibari ambao ndio utambulisha wa Mwananchi yoyote wa kizanzibar pamoja na kuzitambua kazi za sanaa na kuhakikisha vijana wanapata ajira kupitia kazi za sanaa.

Hivyo katika sekta hiyo Wizara inaendelea na Mpango wa kuanzisha chuo cha sanaa kitakachowawezesha vijana kujifunza  sanaa za muziki na kazi za mikono ili kujipatia kipato.

Aidha Wizara imefanikiwa kuandaaa tunzo za wasanii wote ambazo kwa hatua ya awali imeanza na tunzo za  muziki wa aina zote ambazo zitakua na kiasi cha fedha ndani yake kitakachowawezesha wasanii kufungua biashara mbadala na  kuendelea kufanya kazi zaidi za sanaa na kupata mafanikio  kupitia kazi hizo.

Wizara hii chini ya uongozi wa Dkt. Mwinyi imefanikiwa  Kuchukua wasanii wazoefu wa kitaifa na kimataifa kuja kutoa  mafunzo kwa wasanii wa Zanzibar  ili kuwajengea uelewa  juu ya dhana ya kugeuza mziki kuwa biashara.

Wizara inaendelea kuandaa na kuratibu matamasha kwa kushirikiana na sekta binafsi ikiwemo sauti za busara na  tamasha la nchi za jahazi  na kuhakikisha wasanii wa Zanzibar  wanashiriki kuweza kujitangaza na kupata tija.

Wizara imefanikiwa kuongeza bodi ya filamu katika Sensa na filamu ili kuhakikisha wasanii wananufaika na kazi za sanaa zao.

MICHEZO

katika Sekta ya  Michezo Wizara imefanikiwa kuboresha miundombinu ya michezo kama inavyotaka sera ya michezo kwa kuwa na viwanja bora na vya kisasa.

Ndani ya miaka mitatu ya Dkt.Mwinyi Wizara imefanikiwa kujenga kiwanja kipya na cha kisasa cha michezo  eneo la Matumbaku Mjini Unguja ikiwa ni mbadala wa kiwanja cha Malindi ambacho uwekezaji mwengine umechukua nafasi katika eneo hilo.

Katika uwanja mpya wa matumbaku kutakuwa na viwanja viwili vya mipira ya miguu na viwanja vyengne vya michezo tofauti kama mpira wa kikapu na mikono.

Hata hivyo Wizara imefanikiwa  kuuboresha Uwanja wa Amani na  kuufanya  kuwa wa kisasa ambao unakidhi vigezo vya shirikisho la soka la kimataifa  FIFA na Chama cha Mpira wa miguu Barani Afrika CAF.

Miongoni mwa maboresho katika uwanja huo ni uwepo wa kiwanja kikubwa cha ndani (IN DOOR) ambacho kitawezesha kucheza michezo tofauti ikiwemo mpira wa mikono, mpira wa wavu na mpira wa kikapu.

Aidha katika maboresho ya Uwanja huo kutakuwa na ukumbi wa kwanaza wa kimataifa kwa Afrika ambao  utakua na vigezo vya FIFA NA CAF.

Ndani ya miaka hii mitatu Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi aliidhinisha kiasi cha Shiligi bilioni 52 kwa ajili ya maboresho ya Uwanja huo.

Aidha Wizara imefanikiwa kuboresha Uwanja wa Gombani Pemba kwa kuweka nyasi bandia, kubadilisha minara na taa mpya na za kisasa ambazo zitaweza kuhimili na kumuurika eneo la Uwanja na kukwepa ile changamoto ya minara ya kwanza kuwa mirefu na mwangaza kutoka nje na kushindwa kucheza mechi katika nyakati za usiku, jumla ya Shilingi Bilioni 2.8 zimetumika kuboresha Uwanja huo

Wizara imefanikiwa  kurudisha  michezo iliyoachwa kwa muda mrefu ikiwemo michezo ya asili na mchezo  wa ngumi  (boxing) ambao ulisitishwa kuchezwa Zanzibar kwa  zaidi ya miaka 50  sasa.

Ama kweli mitatu inajieleza ni wazi Raisi huyu ametenda mengi naya kupongezwa hivyo sasa kwa pamoja tumpongeze Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi kwa kutekeleza vyema ahadi zake katika kipindi kifupi cha uongozi wake.

 

Hakika Rais Mwinyi ni nahodha anaeiongoza nchi kwa maendeleo yanayoonekana kwa kipindi kifupi cha miaka mitatu.

 

HONGERA DKT. MWINYI.

HONGERA WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.