Habari za Punde

WAZIRI MKUU AFUNGA MAADHIMISHO YA MIKA 50 YA CHUO CHA USTAWI WA JAMII

 

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi baada ya kuwasili kwenye kituo cha mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam kwa lengo la kufunga kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya 
chuo cha Ustawi wa Jamii, Desemba 18, 2023. Wa pili kulia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima.

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akipokea taarifa fupi kutoka kwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima alipowasili kwenye kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere kwa lengo la kufunga Kilele cha Maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo cha Ustawi wa Jamii 
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akimsikiliza Ofisa wa Kampuni ya Coca Cola Kwanza Victor Byemelwa alipotembalea banda la maonesho la Kampuni hiyo kabla ya kufunga Kilele cha Maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo cha Ustawi wa Jamii
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa pamoja na viongozi wengine wakiimba wimbo wa Taifa wakati wa kilele cha Maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo cha Ustawi wa Jamii katika kituo cha mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere
Waziri MKuu, Kassim Majliwa akizungumza alipofunga Maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo cha Ustawi wa Jamii kwenye Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.