Habari za Punde

Waziri wa Afya Zanzibar Mhe.Nassor Mazrui Azungumzia Hali ya Malaria Zanzibar

Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui aakizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na hali ya malaria huko Ofisini kwake Mnazimmoja Mjini Unguja .

Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui aakizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na hali ya malaria huko Ofisini kwake Mnazimmoja Mjini Unguja .

 PICHA NA FAUZIA  MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR

Na Imani Mtuma, Maelezo Zanzibar.

Waziri wa Afya Zanzibar Mhe Nassor Ahmed Mazrui amewataka wananchi kuimarisha usafi katika maeneo yao ili kuondoa mazalia ya mbu wanaosababisha ugonjwa wa malaria.

Akizungumza na waandishi wa habari huko ofisini kwake Mnazimmoja Mjini Unguja amesema endapo jamii itendeleza utamaduni huo itaisaidia serikali kufikia malengo yake ya  kumaliza malaria Zanzibar.

Amesama mashirikano ya pamoja kati ya wizara na wananchi ndio njia pekee ya kumaliza maradhi hayo nchini ,hivyo aliwataka wananchi kuwa na utamaduni wa kuondoa vichaka na madimbwi ya maji katika maeneo yao hasa katika kipindi hichi cha mvua ili kupunguza idadi ya wagonjwa na kuondoa  vifo vitokanavyo  na ugonjwa huo.

Aidha alisema wizara inaendelea na jitihada za kumaliza ugonjwa huo ikiwemo kupiga dawa majumbani  na kutoa vyandarua hivyo aliwataka wananchi kutoa mashirikano wakati wa zoezi hilo na kuendelea kuvitumia  vyandarua ili kujikinga na mbu wanaosababisha ugonjwa huo.

Awali alifahamisha kuwa kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi na muingiliano wa watu  katika  kipindi cha  miezi sita wagonjwa wa  malaria wameongezeka sambamba na vifo viwili vilivyosababbishwa na ugonjwa huo.

Alifahamisha kuwa lengo la serikali zote mbili ni kumaliza kabisa ugonjwa huo na kuwataka wananchi kufuata maelekezo yanayotolewa na  wizara za Afya  juu ya kujikinga na ugonjwa huo ili kushinda vita dhidi ya malaria.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.