Habari za Punde

Uzinduzi wa Barabara za Ndani Tunguu -- Ndijani -- Mkwaju Ngoma Shamrashamra za Miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais Mhe.Harusi Said Suleiman akikukunjua kitambaa kuashiria uzinduzi wa Barabara ya ndani Tunguu-Ndijani Mseweni-Mkwaju Ngoma yenye urefu wa km 7.8 iliyojengwa  kwa kiwango cha lami na kugharimu zaidi ya dola milioni 2 za kimarekani ,katika  shamrashamra za kutimiza miaka 60 ya Mapinduzi.

Na Khadija Khamis – Maelezo .04/01/2024

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mh. Harus Said Suleiman amesema Serikali itaendelea Kuimarisha Miundombinu ya Barabara katika maeneo ya Mjini na Vijini ili kuwaondoshea Changamoto ya Usafiri Wananchi.

 

Ameyasema hayo wakati wa Uzinduzi wa Barabara za ndani Tunguu hadi Ndijani Mseweni, yenye urefu wa kila Mita 7.8, ikiwa ni Shamrashamra za kutimiza miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

 

Amesema Ujenzi huo ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya kuwaletea Maendeleo Wananchi na kutatua Changamoto mbalimbali za Wananchi.

 

Mh, Harusi amempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Dkt. Husein Mwinyi kwa hatua kubwa ya maendeleo aliyofikia ya kuwapatia mahitaji muhimu Wananchi wake.

 

“Mhe Rais Dkt. Husein Mwinyi anakipaji cha Uongozi kwani amepiga hatua kubwa ya maendeleo kwa muda mfupi alipoingia madarakani na kuvuka lengo la utekelezaji kwa zaidi ya asilimia 90, “alisema Mh. Harusi.

 

Hata hivyo aliwataka Wananchi hao kutoa mashirikiano na Serikali kwa kutunza Miundombinu ya Barabara ili iweze kusaidia usafiri na usafirishaji wa bidhaa mbalmbali ili  kujikwamua na Umasikini.

 

Nae Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Shomar Omar Shomar akitoa taarifa ya kitaalamu   amesema Ujenzi wa Barabara ya Tunguu, Mkwajungoma hadi Ndijani Mseweni yenye urefu wa kilo Mita 7.8. imegharimu zaidi ya Dola za   Kimarekani Milioni mbili .

 

Hata hivyo aliwataka Wananchi kuyalinda maeneo ya kuhifadhi Barabara ili kuepusha ajali na kuifanyia uharibifu.

 

Akizungumza kwa Niaba ya Mkuu wa Mkoa wa kusini Unguja, Mhe. Ayoub Muhamed Mahmuod, Mkuu wa Wilaya ya Kati Sadifa Juma Khamis amewashukuru Viongozi wa nchi zote mbili kwa kufuata nyayo za Waasisi wa Mapinduzi  kwa kuwaletea Maendeleo Wananchi kwa Vitendo.

 

Alifahamisha kuwa ujenzi wa barabara za ndani ni Matunda ya Mapinduzi ya miaka 60 hivyo iko haja ya kutunzwa ili zidumu kwa muda mrefu na kuwataka Madereva wenye gari zenye uzito mkubwa wasitumie Barabara hiyo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais Mhe.Harusi Said Suleiman akikata utepe kuashiria uzinduzi wa wa Barabara ya ndani Tunguu-Ndijani Mseweni-Mkwaju Ngoma yenye urefu wa km 7.8 iliyojengwa kwa kiwango cha lami na kugharimu zaidi ya dola milioni 2 za kimarekani katika shamrashamra za kutimiza miaka 60 ya Mapinduzi.
Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais Mhe.Harusi Said Suleiman akitembea katika  Barabara ya ndani Tunguu-Ndijani Mseweni-Mkwaju Ngoma yenye urefu wa km 7.8 iliyojengwa kwa kiwango cha lami  na kugharimu zaidi ya dola milioni 2 za kimarekani mara baada ya kuizindua katika shamrashamra za kutimiza  miaka 60 ya Mapinduzi.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya ujenzi , mawasiliano na uchukuzi Mhandisi shomari omari shomari akitoa maelezo ya ujenzi wa Barabara ya ndani Tunguu-Ndijani Mseweni-Mkwaju Ngoma iliyojengwa kwa kiwango cha lami wakati wa uzinduzi wa mradi huo ikiwa ni miongoni mwa  shamrashamra za kutimiza miaka 60 ya Mapinduzi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais mhe.Harusi Said Suleiman akihutubia mara baada ya kuzindua  Barabara ya ndani Tunguu-Ndijani Mseweni-Mkwaju Ngoma iliyojengwa kwa kiwango cha lami yenye urefu wa km 7.8 na kugharimu zaidi ya dola  mil.2 ikiwa ni shamrashamra za kutimiza miaka 60 ya Mapinduzi

Baadhi ya Vijana wa ndijani mseweni wakifuatilia na kufurahia uzinduzi wa barabara ya ndani wa Barabara ya ndani Tunguu-Ndijani Mseweni-Mkwaju Ngoma iliyojengwa kwa kiwango cha lami na kugharimu zaidi ya dola  mil.2 za kimarekani ikiwa ni  shamrashamra za kutimiza  miaka 60 ya Mapinduzi.
PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR 


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.