Na Rahma Khamis Malezo Zanzibar.
Mfuko wa huduma za afya Zanzibar wametiliana saini na Taasisi ya Pharm -Acess makubaliano ya ushirikiano ili kuimarisha utendaji kazi katika mfuko huo.
Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika Ofisi za ZSHF Michenzani Mall Kaimu Mkurugenzi Mkuu Yaasin Ameir Juma amesema makuibaliano hayo yatasaidia kuimarisha upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wote.
Amesema makubaliano hayo ni pamoja na kushirikiana katika kusajili sekta isiyo rasmi na kuhakikisha upatikananji wa rasilimali za kutosha na kushirikiana katika maeneo ya kitaamu ili kuimarisha mfuko huo na kuendelea kutoa huduma bora kwa wazanzibar .
“mashirikiano kati yatu na taasisi ya Pharm -Acess ni ya muda mrefu kuanzia kuusarifu mfuko huu hadi kufikia hapa tulipo hivyo tunaendelea kushirikiana nasi ili kuendeleza utoaji wa huduma bora za afya kwa jamii” alifahamisha Kaimu Yaasin.”
Akigusia suala la kuendelea na usajili wa makundi mengine Kaimu Mkurugenzi amesema hivi karibumi wanatarajia kuanza usajili wa wanachama wa sekta binafsi ambapo Pharm-Acess wamekuja kuunga mkono ili usajili huo uweze kukamilika kwa haraka.
Nae Mkurugenzi Mkaazi wa Taasisi ya Pharm-Acess Heri Marwa amefahamisha kuwa ushirikiano uliopo kati yao ndio umesaidia uwepo wa mfuko huo na kuwaomba wananchi kuutumia mfuko ipaswavyo ili kupata huduma bora na za uhakika.
Aidha ameongeza kuwa Taasisi hiyo imekuwa ikifanya kazi na sekta mbalimbali za Serikali ikiwemo afya ili kuhakikisha wanafikia malengo waliyojiwekea.
Hata hivyo Mkurugenzi Marwa amesema watahakikisha kuwa watu ambao hawana uwezo na wanaishi katika mazingira magumu wanapata huduma kupitia mfuko huo ili kuboresha afya zao.
Itakumbukwa kwamba Mfuko wa Huduma za Afya Zanzibar umeanza usajili wa wananchama wake kupitia Sekta rasmi na kusema kuwa usajili wa sekta zisizo rasmi na makundi maalum utanza mara baada ya kukamilika kwa usajili wa sekta rasmi.
No comments:
Post a Comment