TAARIFA KWA UMMA KUHUSU RATIBA YA MAZISHI YA
KITAIFA YA RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA PILI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA HAYATI
ALHAJI ALI HASSAN MWINYI
Ndugu Wananchi na Watanzania wenzangu;
Kama tulivyojulishwa na
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwamba Rais Mstaafu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Ali
Hassan Mwinyi, amefariki jana tarehe 29 Februari, 2024 saa 11.30 Jioni
katika Hospitali ya Mzena,
kwa masikitiko makubwa, ninaomba kuungana na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoa Salamu za Pole kwa Mheshimiwa Dr Hussein Ali Hassan Mwinyi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, wanafamilia na Watanzania wote kwa msiba huu mkubwa wa kiongozi wetu mpendwa.
Ndugu Wananchi na Watanzania wenzangu;
Kufuatia msiba huu, Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ametangaza maombolezo ya siku saba na bendera kupeperushwa nusu mlingoti
kuanzia leo tarehe 1 Machi, 2024. Katika kipindi hiki cha siku saba za
maombolezo, Taifa litaungana kwa pamoja na wanafamilia katika maombolezo na
mazishi ya Kitaifa yatakayofanyika huko Unguja Zanzibar kwa ratiba ifuatayo;.
1.
Ijumaa tarehe 01 Machi, 2024;
i.
Saa 3:00 Asubuhi;
Milango ya uwanja wa Uhuru itakuwa
wazi kwa ajili ya Wananchi kuingia kwa ajili ya maombolezo.
ii. Kuanzia Saa 4:00 Asubuhi;
Viongozi mbalimbali kuwasili uwanja
wa Uhuru kwa ajili ya Maombolezo ya Kitaifa na Kuaga mwili wa Hayati Ali Hassan Mwinyi
iii. Kuanzia Saa 5:30 Asubuhi;
Mwili wa Hayati Mzee wetu Ali Hassan
Mwinyi kuondoka nyumbani Mikocheni kuelekea Msikiti Mkuu wa BAKWATA uliopo Kinondoni
ambako Sheikh Dokta Abubakar Bin Zuber Bin Ali ataongoza swala ya Ijumaa pamoja
na taratibu zote za kidini.
Mwili wa Hayati Ali Hassan Mwinyi
kuelekea Uwanja wa Uhuru.
·
Dua na maombi kutoka kwa viongozi wa dini
·
Salamu za rambirambi kutoka kwa viongozi mbalimbali;
·
Viongozi na Wananchi mbalimbali kutoa heshima
za mwisho
vi. Saa 11:00 Jioni;
Mwili wa Hayati Ali Hassan Mwinyi, kuondoka
uwanja wa Uhuru kuelekea uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage
Nyerere;
Wananchi wa Jiji la Zanzibar na maeneo mengine
ya Unguja kupokea Mwili wa Hayati Ali Hassan Mwinyi, katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Abeid Aman Karume na kuelekea nyumbani kwa marehemu.
Milango ya uwanja wa Amani itakuwa
wazi kuanzia saa 12:00 asubuhi ambako Shughuli ya kitaifa itafanyika.
Viongozi mbalimbali kuwasili uwanja wa
Aman kwa ajili ya Maombolezo
ya Kitaifa na Kuaga mwili wa Hayati
Ali Hassan Mwinyi
Mwili wa Hayati Ali Hassan Mwinyi
kuondoka nyumbani kwa marehemu kuelekea Uwanja wa Aman.
Dua na swala kutoka kwa viongozi wa
dini
· Salamu
za rambirambi kutoka kwa viongozi mbalimbali
·
Salamu
za Pole kutoka kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Viongozi na Wananchi mbalimbali kutoa
heshima za mwisho
Mwili wa Hayati Ali Hassan Mwinyi
uwanja wa Aman kuelekea kijijini kwa marehemu Mangapwani kwa ajili ya mazishi ya Kitaifa
viii. Saa 10:00 Mchana
Wananchi na Viongozi mbalimbali
kushiriki Mazishi ya Kitaifa ya hayati Ali Hassan Mwinyi eneo la Mangapwani.
Ndugu Wananchi na Watanzania wenzangu;
Watanzania
tumepokea taarifa za msiba wa mzee wetu, kiongozi wetu Rais Mstaafu
wa awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa masikitiko makubwa na Mheshimiwa
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametutaka Watanzania wote kuwa watulivu na
wastahimilivu kutokana na kifo cha mpendwa wetu.
INNA LILAHI WA INNA ILAYHI RAJI’ UN
SISI SOTE NI WA MWENYEZI MUNGU NA KWAKE TUTAREJEA
No comments:
Post a Comment