Habari za Punde

Zara ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Othman Masoud Soko la Marikiti Darajani Unguja leo

  

Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman akiangalia bei za ndizi za Mkono mmoja katika duka la mfanyabiashara Haji Juma Vuai wa Soko Kuu Darajani. Mhe. Othman alitembelea soko hilo leo JAlkhamis tarehe 28.03.2024 kuangali hali ya bidhaa upatikanaji wake pamoja na bei za bidhaa mbali mbali hasa kipindi hiki cha Ramadhan
Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman akisalimiana na  mtaali Bi. Caw sylus wakati walipokutana huko katika soko kuu la darajani wakati mhe makamu alipofanya  ziara  katika masoko mbali mbali kuangalia bei za bidhaa mbali mbali leo Alkhamis tarehe 28.03.2024

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman (kulia), wakizungunza pamoja na mfanyabiashara wa majimbi Shekh . Omar Hamad huko katika soko la Mwanakwerekwe C wakati Mhe. Makamu alipokuwa kwenye ziara ya kutembelea masoko m bali mbali ya mkoa wa mjini Magharibi laeo tarehe 28.03.2024. Picha na ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar

 

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman masoud Othman akisalimiana na Mkuu wa wilaya ya Mjini Mhe. Rashid Simai Msaraka wakati mhe. Makamu akiingia katika viwanja vya soko la Kibandamaiti  mkoa wa mjini Mgharib katika ziara yake aliyoifanya leo tarehe 28.3.2024 kuangalia bei za bidhaa mbali mbali na upatikanaji wake. Picha na ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud amewataka watendaji katika masoko mbali kujitahidi kuweka mazinira ya usafii katika maeneo yote ya bisara tofauti ili kuepusha madhara ya afya za wananchi  yanayoweza kupatikana kutokana na kutumia vyakula vinavyouzwa katika hali ya uchafu unaoweza kuepukika.

Mhe. Othman ameyasema hayo mara baada ya kukamilisha ziara ya kuyatembelea masoko mbali mbali katika mkoa wa mjini magharib kuona hali halisi ya upatikanaji wa bidhaa  pamoja na bei zake hasa katika kipindi hiki cha mfungo wa  mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Amefahamisha kwamba masoko mengi katika mkoa huo wa mjini Marib yanayouzwa bidhaa za nafaka , matunda, samaki pamoja na nyama na mboga mboga yanakabiliwa na hali ya uchafu ikiwemo maji yanayotirika na kusababisha  hali ya unyevu nyevu huku  wafanyabiashara wakiendelea na shunguli  zao katika hali hiyo jambo ambalo ni hatari kwa afya ya mtumiaji.

Amefahamisha kwamba hali hiyo ni jambo linalohitaji kuzingatiwa katika kuhakikisha kwamba kunawekwa na kudumishwa usafi wa mazingira katika maeneo yote yanayoendelea na shughuli za biashara za aina zote angalau kwa kumwaga kokoto ili kupunuza athari zinazoweza kusababishwa na hali ya uchafu.

Akizungunzia bei za bidhaa mbali mbali Mhe. Othman amesema kwamba bidhaa nyingi bei ziko juu ikilinganishwa na hali halisi ya kipato cha wananchi jambo ambalo linasababishia wananchi kuendelea kukubwa na ukali wa maisha.

Hata hivyo, amesema kwamba licha ya hali ya bei kuwa juu lakini bidhaa nyingi za mahitaji ya wananchi hasa katika kipindi hiki cha mfungo wa ramadhani zinapatikana kwa wingi katika masoko yote nchini.

Mapema baadhi ya wafanyabiashara hasa wa kitoweo cha nyama walimueleza mhe. Makamu kwamba bei ya bidhaa hizo zimepanda kwa kuwa ngombe wengi na mbuzi hulazimika kuaizwa kutoka Tanzania bara kwa vile Zanzibar  haina  mifugo ya kutosheleza mahitaji ya  soko la walaji huku kukiwa kumepanda ushuru na ada mbali mbali za kuiniza mifugo hiyo apa Zanzibar.

Aidha wamemuomba mhe. Kwamba serikali izinatie sana hali ya upatikanaji wa mikopo ili waweze kuwa na ustawi imara wa kuendesha suuli zao za biashara  katika masoko na kwa bidhaa mbali mbali jambo lityakalowasaidia kumudu kupambana vyema na hali ya maisha.

Pia wafanya biashara hao wa meomba serikali kuangalia ya bei ya ukodishwaji wa Milango na wote kurejeswa katika seemu zao za biashara baada ya ujezi wa ujenzi wa masoko mbali mbali unaoendelea  kukamilika  hasa kwa kuzingatia kwamba wengi wao wamepoteza mitaji yao ya biashara kutokana na  hali ya biashara kuwa ngumu.

Mapema Mhe. Alitembelea soko la Mwanakwerekwe C, Soko la Mwanakwerekwe raound abaut , soko la Kibanda Maiti pamoja na soko kuu la darajani kuona hali halisi ya bei mbali mbali za bidhaa na upatikanaji wake hasa katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa ramadhani .

Imetolewa na ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar kupitia kitengo cake cha  habari leo  Alkhamis Maci 28, 2024..

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.