Habari za Punde

MAONESHO YA KAZI ZA MAABARA YAENDELEA ZANZIBA

 


Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hassan Khamis Hafidh akipata maelezo kutoka kwa Afisa Maabara Kemikali kutoka Taasisi  ya viwango ZBS Sahiya  Abdalla Khamis alipotembelea maonesho ya kazi za maabara huko viwanja vya Kisonge Mjini Unguja ikiwa ni wiki ya maabara ambayo hufikia kilele chake kila ifikapo April 21 duniani kote.

Na Rahma Khamis Maelezo              17/4/2024

 

Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe Hassan Khamis Hafidh amewataka wataalamu wa maabara kutoa huduma   kama  wanazozitoa katika manyesho ili wananchi wapate huduma bora .

 

Ameyasema hayo wakati alipotembelea mabanda ya maonesho ya kazi za maabara katika Uwanja wa Kumbukumbu Kisonge wilaya ya Mjini  ikiwa ni wiki  ya maabara iliyoanzia April 16.

 

Amesema Wizara imejipanga kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma za uhakika hivyo amewataka wataalamu hao kuendelea kutoa huduma katika taasisi zao kama alivyoziona katika maonesha hayo.

 

“Huduma mnazozitoa hapa ni nzuri sana mweyewe nimeona nakuombeni muendelee kuzitoa huduma hizi katika taasisi zenu  ili wananchi wasilalamike kuwa wamekosa huduma,” alisisitiza Naibu Waziri.

  

Nae Afisa Mtaalamu wa Maabara kutoka Baraza la wataalamu Time Hassan  amesema kuwa kwa kushirikiana na wizara ya afya wameshiriki maonesho hayo   ili  jamii iweze kutambua kazi zinazofanywa na maabara pamoja na umuhimu wake.

  

Kwa upande wake Afisa Mhamasishaji Mpango wa Damu Salama  Dokt Omar Said Omar amewahamasisha wananchi kujitokeza kuchangia damu kwa lengo la kuawasaidia wengine.

 

“Sisi kama Kitengo tutahakikisha wananchi wanapima na kuchangia damu kwa wale wenye vigezo ili kuokoa maisha ya watu wanaohitaji kwa vile damu ndio kila kitu katika maisha yetu,”alisisitiza Dkt Omar.

 

Akizungumzia kuhusu vigezo vya kuweza kuchangia damu  Dkt Omar amefafanua kuwa kwa mwanamme  lazima awe na wingi wa damu  usiopungua 13 .5 ambapo kwa mwanamke ni 12.5  na asiwe na maradhi endelevu.

 

Maadhimisho ya siku ya Maabara Duniani hufanyika kila ifikapo April 21 ambapo Kaulimbiu ya mwaka huu ni “Maabara ni Kila Kitu” 

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.