Habari za Punde

Dkt.Biteko : Wauguzi ni Kada Muhimu kwa Maendeleo ya Huduma za Afya Nchini

 

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt Doto Biteko akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani yaliyofanyika Jijini Tanga ambapo alimwakilisha Rais Dkt Samia Suluhu.

Na Oscar Assenga, TANGA
NAIBU Waziri Mkuu Dkt Dotto Biteko amefunga kilele cha  maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani huku akieleza wauguzi ni kada muhimu kwa sababu maendeleo ya huduma za afya nchini hayawezi kufikiwa bila uwepo wao.

Dkt Biteko ambaye pia ni Waziri wa Nishati aliyasema hayo leo wakati akifunga maadhimisho hayo yaliyokuwa yakiendelea kwenye ukumbi wa Hotel ya Regail Naivera Jijini Tanga ambapo alimwakilisha Rais Dkt Samia Suluhu.

Alisema kwamba wauguzi wanafanya nzuri na kwamba asilimia 100 ya watumishi wa sekta ya afya nchini asilimia 60 ni wauguzi na shughuli zinazowapeleka kazini watoa huduma za afya asilimia 80 ya kazi hizo zinafanywa na wauguzi lakini changamoto zilizongumza na wauguzi niungane nanyi ni za kweli ni lazima kuona namna ya zifanyiwe kazi.

“Leo mnaposheherekea siku ya wauguzi mnakazi kubwa ya kukumbushana wajibu wenu na kurejea viapo vyenu mtumie siku ya leo muendelee kukumbushana kutekeleza wajibu wenu”Alisema

Aidha aliwaambia kwamba wao ni kundi muhimu na wanatambua mchango wao kwa jamii na kwamba hata watoto wanapozaliwa mtu wa kwanza kumpokea mkononi hata kaba ya mzazi ni muunguzi.

“Watu wanakuja kwenu wakiwa na maumivu wengine wamezimia kutokana na maradhi mbalimbali waliyyapata wengine kwa ajali wanakuja wakiwa na tumaini moja tu afya zao na maumivi yao kuwatoka wanawategemea nyie hivyo muuguzi ukimtaja kuwa daraja la pili utakuwa umetenda dhambi “alisema

“Niwahakikishie kwamba Serikali inatambua mchango wenu kama wauguzi wapo asilimia 60 na ndio wanafanya kazi asilimia 80 ni kweli lazima miundo yenu tuiangalie hivi ni sayansi gani inayohusika na utawala ambayo muuguzi mwenye uzoezi mkubwa kwenye sekta hawezi kuwa kiongozi kwenye eneo la uongozi?Alisema

“Kwamba zipo taaluma ambazo mtu atasoma kazi yake ni kuuongozwa na hawezi kupata nafasi ya kuongoza na hata ikitokea kwa wauguzi wenzake hilo jambo sio sawa hivyo Naibu Waziri wa Afya nielekeze hilo jambo mlifanyia kazi mliangalie sitaki kuingilia misingi taaluma lakini nazungumzia logiki ya kawaida ya misingi ya utawala lazima haki ya uongozi kuna watu wengine wanaipata “Alisema Naibu Waziri Mkuu.

“Kama kuna kiongozi mzuri wa uongozi anauwezo wa kufanya kazi vizuri kwanini umuondoe kwenye vikao vya uongozi kwa sababu eti yeye ni muuguzi na uuguzi ugeuke kuwa ni mtu wa kutumwa na kushurutishwa na mtu mwengine jambo hilo sio sawa”Alisisitiza Naibu Waziri Mkuu Dkt Biteko.

Awali akizungumza Naibu Waziri wa Afya Dkt Godwin Molel aliwataka watumishi wasikubali kugawanywa hakuna cha nesi, daktari, maabara na kada nyengine kwani wao ni kitu kimoja.

“Kwa sababu kila mtu anaweza kuwa DMO kwenye suala la uongozi lakini uthibiti namba moja imetokea wizara ya afya wametokea mawaziri maprofesa lakini amekuja dada yetu mwanasheria Ummy Mwalimu leo na anafanya vizuri sana tunahaangaika kuna wauguzi na wakunga msikubali watu wawatawale ishu tupige mzigo Dkt Samia atape kura zake nyie mnaonaje hiyo”Alisema Dkt Molel

Katibu Mkuu wa Chama cha Wauguzi Tanzania Samweli Mwambopa alisema kwamba wanaishukuru Serikali katika kuboresha sekta ya afya nchini kiwemo ujenzi wa miundombinu, uwekezaji vifaa tiba ambayo ndio msingi wa utoaji wa huduma bora za afya.

Alisema kauli mbiu ya maadhimisho hayo inawakumbusha viongozi wa Serikali na wananchi kwamba wanapowekeza kwenye uuguzi unasaidia kuboresha huduma za afya na kuwepo kwa huduma bora.

Aidha alisema huduma bora katika Hospitali kwa asilimia 80 hutegemea huduma za uuguzi ndio maana wanahimiza kufanya uwekezaji kwenye eneo hilo kwenyey sekta ya afya na kutambua hiyo ni taaluma inayojitegemea.

Hata hivyo alisema wauguzi wapo mstari wa mbele kuhakikisha wananchi wanapata huduma wakati wote hivyo wapo kwenye kutoa ufumbuzi katika kusaidia wagonjwa.

Alisema mafaniko ya chama hicho ni wauguzi wamekuwa mstari wa mbele kutoa huduma za VVU ikiwemo kutoa ushaauri nafasi upimaji na uanzishaji wa dawa kwa wapokea huduma. 
NAIBU Waziri wa Afya Dkt Godwin Molel  akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani yaliyofanyika Jijini Tanga ambapo alimwakilisha Rais Dkt Samia Suluhu 
MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani yaliyofanyika Jijini Tanga ambapo alimwakilisha Rais Dkt Samia Suluhu 
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Rajabu Abdurhaman akizungumza 


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.