Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman amesema kwamba kuwepo miundombinu imara na sahihi katika shughuli zozote za kibiashara ni jambo la lalazima ili kuwezesha shughuli hizo kufanyika vyema na kuleta tija kubwa kwa serikali na wafanyabiasara husika.
Mhe. Othman ambaye pia ni Mwenyikiti wa Taifa wa Chama cha ACT wazalendo ameyasema hayo huko
katika soko la Machinga mjini Tabora i
alipotembelea soko la wafanyabiashara hoa na kusikiliza kero mbali mbali
walizonazo baada ya kuwatembelea.
Amefaamisha kwamba ni jukumu la mamlaka zinazohusika na
kusimamia shughuli za biashara
kuaakikisha kwamba wanteneneza
mazingira wezeshi ya kibiashara ili kuweza kuwavuta wateja wa biasara sambamba
na kulinda usalama wa mtumiaji.
Amesema kwamba serikali inawajibu wa kutayuarisa sera na
mipano bora kwa kuwawezesa wafanyabiasara ndoo ndoo kujiajiri na kuhakikisha
kwamba inakuwepo misingi bora na imara
ili waweze kuenesa kazi zao katika maeneo salama hasa kwenye biashara za vyakula ambazo zinaahitaji
usafi na unadhifu mkubwa ili kulinda pia afya ya mlaji.
Mapema wafanyabiashara wadogo wadogo wa soko hilo maarufu la wamachinga la mjini Tabora walimueleza Mhe. Ohtman
kwamba soko hilo limejengwa kwa kuondosha njiani na kusababisha wafanyabiashara
hao kutokukua na mazingira na mahali sahihi
pa kufanyia biashara kwa muda mrefu sasa .
Wamedai kwamba ali iyo imewafanya kukata mitaji yao ya
biasara uku wakuendendelea kuwa na madeni ya benki kwa kusindwa kulipa kutokana
na mitaji iyo kukosa faida na kufa kabisa kulikosababiswa na kokosa wateja kwa
vile soko ilo alina mazinira rsafiki ya kuwavuta wateja.
Walimuomba Mhe. Othmani kuwapelekea kilio chao kwa Rais wa
Jamuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan cha kukosa sehemu ya
biashara huku baadhi yao wakishindwa
kulipa mikopo ya Benki waliyokopa kuendesha biashara hizo.
Wamesema kwamba viongozi mbali mbali wa nazi tofauti wamewai
kufika na kupokea kilio chao lakini ati sasa hakuna mabadiliko yoyote yaliweza kufanywa na
serikali ya krekebisa mazingira hayo .
Wameiomba serikali kutenga
bajeti na kufanya jitiada za kulijena soko hilo kwendana na mazinira
bora ya biasara na serikali iweze kukusanya kodi zitokanazo na ada na ushuru wa
aina mbali mbali kutoka kwa wafanyabiashara wa hapo.
Katika atua nyengine
Mhe. Othman , alizindua mashina,
matawi, na ofisi za Jimbo la ACT
la Jimbo la Tabora mjini ambapo aliwataka kukiuna mkono chama hicho
ili kuendeleza jitiada za kuzitumia rasilimali mbali mbali za ndani
katika kukuza uchumi na kuondosha umasikini kwa wananchi.
Amesema kwamba Chama hicho
kimejipana kufanya mageuzi ya kiucumi na kimaendeleo kwa wananchi wa
Tanzania na kuwataka kukiunga mkono kwa kuhakikisha wanawachugua viongozi kutoka
chama hico wa serikali za vijiji na mitaa katika uchaguzi wa baadae mwaka huu.
Mhe. Othman amemaliza ziara yake katika mkoa Tabora aliwasili
mkoani Kahama kuendelea na ziara yake katika Mkoa wa Shinyanga anatarajiwa
kumaliza ziara yake katika Mkoa kabla ya kurejea Zanzibar mwishoni mwa wiki hii.
Mwisho
Imetolewa na ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
kupitia Kitengo chake cha habari leo Jumatano tarehe 08.05.04.
No comments:
Post a Comment