Na Jumanne Magazi
Mkurugenzi Mkuu wa shirika la ndege Tanzania (ATCL) Mhandisi Ladislaus Matindi,amesema wanatumia maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba kama sehemu ya kuelimisha jamii kuhusu usafiri nchini,kuuza za bidhaa za shirika hilo pamoja na kupokea maoni.
Mhandisi Matindi,ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye Banda la ATCL lilopo kwenye maonesho ya Sabasaba.
Amesema pia kupitia maonesho hayo wananchi watapata bidhaa zote ikiwemo kununua tiketi za ndani na nje.
"Tumejitaidi kutoa elimu na huduma,hapa kuna bidhaa ya kibubu ambayo utaweka hela kidodogo mpaka utakapomaliza hela ya tiketi,yote tunafanya haya ili kumrahishia mteja"Amesema Mhandisi Matindi.
Aidha,Mhandisi Matindi,amesema kwa sasa shirika hilo wanahuduma ya kuwatambua wasafiri wa mara kwa mara ndege za ATCL kwa kupata huduma ya Upendeleo ikiwemo kupata tiketi za hadhi ya juu.
Hata hivyo,Mhandisi Matindi,amesema kwa sasa wanajivunia kuwepo kwa ndege za mizigo huku akiwakaribisha wafanyabiashara kutumia huduma hii.
Sanjari na hayo,MhandisiMatindi,amesadma kwa sasa wanajitihada za kuwavutia vijana wadogo waweze kushiriki kwenye sekta ya Anga.
No comments:
Post a Comment