Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Mwinyi Amewaapisha Makatibu Wakuu Aliyewateua Hivi Karibu

MAKATIBU Wakuu wateule walioteuliwa hivi karibuni wakiwa katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar wakisubiri kuapishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, hafla hiyo ya uapisho iliyofanyika leo 24-8-2024 Ikulu Zanzibar. 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Dkt. Habiba Hassan Omar kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar, hafla hiyo ya uapisho iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 24-8-2024
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Ndg. Khamis Suleiman Mwalim kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Kazi,Uchumi na Uwekezaji Zanzibar, hafla hiyo iliyofanyika leo 24-8-2024 katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Dkt.Mngereza Mzee Miraji kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar, hafla hiyo ya uapisho iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 24-8-2024
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mariam Juma Abdalla Saadalla kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais,hafla hiyo ya uapisho iliyofanyika leo 24-8-2024 katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar
BAADHI ya Wageni waalikwa katika hafla ya uapisho wa Makatibu Wakuu walioteuliwa hivi karibuni, wakifuatilia hafla hiyo wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akiwaapisha katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 24-8-2024.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amewaapisha makatibu wakuu wanne aliowateua hivi karibuni.

Hafla ya uapisho huo ilifanyika Ikulu, Zanzibar kwa kuratibiwa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena Ahmeid Said.

Walioapishwa ni Dk. Habiba Hassan Omar, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi ambae amechukua nafasi ya aliekua katibu wa Wizara hiyo, Dk. Mngereza Mzee Miraji alieteuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya. Awali Dk. Habiba alikua Katibu Mkuu Wizara ya Afya.

Rais Dk. Mwinyi pia amemuapisha Dk. Mngereza Mzee Miraji kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, kabla ya nafasi hiyo, Dk. Miraji alikua Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi.

Pia Dk. Mwinyi amemuapisha ndugu Maryam Juma Abdalla Saadalla kuwa Katibu wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, kabla ya nafasi hiyo Maryam alikua Katibu Mkuu (Kazi na Uwezeshaji) katika Ofisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji.

Aidha, Rais Dk. Mwinyi amemuapisha Khamis Suleiman Mwalim kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji. Kabla ya nafasi hiyo, Khamis alikua Katibu Mkuu (Uchumi na Uwekezaji) katika Ofisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji.

Hafla ya uapisho huo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, wakiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Sulemain Abdulla, viongozi wa dini pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama.

IDARA YA MAWASILIANO, IKULU ZANZIBAR

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.