Kaimu Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB akimkabidhi Hundi ya Tshs Milioni 50 Katibu Mkuu, Wizara wa Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo Ndg Fatma Hamad Rajabu ikiwa ni udhamini wa Kombe la Mapinduzi hafla iliyofanyika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo,Migombani .
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB. Ahmed Nassour akimkabidhi Track Suit 100 Katibu Mkuu, Wizara wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Ndg Fatma Hamad Rajabu ikiwa ni mchango wa kudhamini siku ya Mazoezi Kitaifa yatayofanyika kisiwani Pemba hafla iliyofanyika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Migombani .
Katibu Mkuu, Wizara wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Ndg Fatma Hamad Rajabu ameipongeza Benki ya NMB kwa kuiunga mkono Serikali katika shughuli za maendeleo ikiwemo michezo.
Ameyasema hayo wakati wa Makabidhiano ya Track Suit na Hundi ya Tshs Milioni 50 iliyotolewa na Benki ya NMB ikiwa ni mchango wa kudhamini siku ya mazoezi Kitaifa na Kombe la Mapinduzi hafla iliyofanyika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Migombani.
Amesema mchango huo utasaidia mustakbali mzima wa michezo pamoja na kutoa hamasa kwa wachezaji katika mashindano ya Kombe la Mapinduzi ambayo yanatarajiwa kuanza January 03 .2025 .
Aidha amesema katika mashindano hayo Timu ya Kimataifa zinazoshiriki mashindano ya Chan zitakuwepo pamoja na wazawa wa Zanzibar Herous .
Katibu huyo amempongeza Waziri wa Habari Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita kwa kazi kubwa anayoifanya kuisimamia na kuiongoza Wizara hiyo.
Nae Kaimu Mtendaji wa Benki ya NMB Kanda ya Zanzibar Ahmed Nassour amesema mchango wa track suit 100 utasaidia kuhamasisha mazoezi pamoja na kutoa hamasa katika siku ya mazoezi kitaifa ili kufanikisha shamrashamra ya Maadhimisho ya miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Amesema NMB ni miongoni mwa wadau wakubwa katika shughuli mbali mbali za kimaendeleo kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Amefahamisha kuwa Benki hiyo itaendelea kutoa mashirikiano kwa Serikali ili kuhakikisha unaimarisha mustakbali ya michezo na afya kwa Wazanzibar.
Ameeleza kwamba katika miaka 12 mfululizo Benki ya NMB inaunga mkono Serikali katika kudhamini michezo jambo ambalo linaonyesha kuwajali wananchi wao.
Imetolewa na Kitengo cha Habari Mawasiliano na Uhusiano.
WHVUM.
No comments:
Post a Comment