Habari za Punde

Ufinguzi wa Kongamano la Vijana Kuwejengea Uwezo Kupata Maendeleo


Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Vijana Zanzibar Shaibu Ibrahim Mohammed amesema Serikali itaendelea kubuni mbinu mbalimbali za kuwajengea uwezo Vijana ili waweze kupata maendeleo.

Ameyasema hayo wakati alipokuwa akifunguwa Kongamano la Vijana huko Katika kituo cha Maendeleo ya Vijana Bweleo Wilaya ya Magharibi B.

Amesema Kongamano hilo ni muhimu katika kuwapa moyo wa kujitolea na uzalendo Vijana hasa katika kipindi hiki cha kuharakiza maendeleo ya Nchi.

Aidha amesema Wizara ipo pamoja na Wadau wa masuala ya Vijana ikiwemo kupatia mafunzo ya Uongozi ili waweze kuwa Wazalendo wa kujenga Nchi yao na Viongozi wa hapo baadae.

Hivyo amewaomba Wadau wa Maendeleo kuendelea kushirikiana na Wizara hiyo ili kuwaendeleza na kuwawezesha Vijana katika nyanja mbalimbali kama vile za kijamii, kisiasa na kiuchumi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya (PPIZ), inayojishughulisha na kilimo hai na masuala ya kijamii Ikram Ramadhan Soraga amesema wapo mstari wa mbele kuwajengea uwezo vijana katika masuala ya kuijitolea na Uongozi.

Hata hivyo amesema kongamano hilo ni muhiumu kwa Vijana kwani yatasaidia kuweza kujielewa, kuwajengea uwezo na kuweza kujiajiri na kuajiriwa.

Nae Faiza Nassor Said, Mratibu wa ZAN change Makers amesema lengo la mradi huo ni kuwakusanya Vijana kutoka maeneo mbalimbali ya Zanzibar na nje ya Nchi ili waweze kujitambua, kujiongoza na kuelewa jinsi ya kuishi na Watu wengine.

Mafunzo hayo ya siku 4 ya kuwajengea uwezo Vijana kutoka Tanzania bara, Ghana na wenyeji Zanzibar, yameandaliwa na Taasisi ya ZAN Change Makers chini ya Ufadhili wa mashirika mbalimbali ikiwemo USAID na IRI.

Imetolewa na Kitengo Cha Habari, Mawasiliano na Uhusiano,

WHVUM 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.