JAJI Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Khamis Ramadhan Abdallah, akipata maelezo kuhusu Tume ya Haki za Binaadamu na Utawala Bora (THBUT), alipotembela banda la tume hiyo, viwanja vya Mapindizi Square, Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi, kwenye maonesho ya wiki ya Sheria, ikiwa ni mwendelezo wa matukio ya siku ya Sheria (Law day), iliyoanza tangu Januari 31 mwaka huu.
JAJI Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Khamis Ramadhan Abdallah, akisaini kitabu cha wageni, kwenye banda la Tume ya Haki za Binaadamu na Utawala Bora (THBUT), ambayo imeshitiki maonesho ya wiki ya Sheria, ikiwa ni mwendelezo wa matukio ya siku ya Sheria (Law day), viwanja vya Mapindizi Square, Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi.Ofisa wa Tume ya Haki za Binaadamu na Utawala Bora (THBUB), Fatma Serembe Khamis, akisikiliza malalamiko ya Bw. Saleh Khamis Saleh, mkaazi wa Chumbuni Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi aliefika kwenye banda hilo, kuwasilisha malalamiko yake. Kupokea malalamiko ni moja kati ya kazi za THBUB ambayo imeshiriki maonesho ya wiki ya Sheria, ikiwa ni mwendelezo wa matukio ya siku ya Sheria (Law day), viwanja vya Mapindizi Square, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Jaji wa Mahkama Kuu ya Zanzibar, Fatma Hamid Mahmoud, akipokea maelezo kuhusu Tume ya Haki za Binaadamu na Utawala Bora (THBUB) kutoka kwa Ofisa wa Tume hiyo, Fatma Serembe Khamis alipotembelea banda la THBUB kwenye maonesho ya wiki ya Sheria, viwanja vya Mapindizi Square, Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi, ikiwa ni mwendelezo wa matukio ya siku ya Sheria (Law day).
No comments:
Post a Comment