Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt,Hussein Ali Mwinyi amesema Chama cha Mapinduzi [CCM] kinaandaa Mpango Mkakati Maalum kuhakikisha Jumuiya za Chama hicho zinakuwa na nguvu ya kujitegemea na Miradi Mikubwa ya Maendeleo.
Dkt,Mwinyi ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ametoa tamko hilo alipozungumza baada ya kuweka jiwe la msingi la Bweni la Vijana wa Kiume wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi [UVCCM].
Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa ni lazima Chama nacho kiache alama ya uongozi itakayokumbukwa kwa muda mrefu kwa kufanya mambo makubwa ya maendeleo na miradi ya Chama katika ngazi zote.
Makamu Mwenyekiti huyo wa CCM Zanzibar amefahamisha kuwa Alama iliyoachwa na Serikali katika Sekta zote za Maendeleo ni lazima pia iachwe ndani ya CCM.
Dkt,ameipongeza UVCCM kwa kufanikiwa kujenga Jengo hilo litakalotumika kwa harakati mbalimbali za Jumuiya hiyo.
Aidha amesema Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kuunga Mkono juhudi za Jumuiya hiyo kwa hali na Mali ili dhamira ya kuwajenga vijana kuwa wazalendo na kuwapatia mafunzo mbalimbali ifanikiwe.
Dkt,Mwinyi ameisisitiza UVCCM kuendeleza kasi ya uhamasishaji uandikishaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura na kuhakikisha vijana wengi wanajiandikisha litakapoanza kwa upande wa Unguja hivi karibuni.
Ametoa wito kwa vijana kutobaki nyuma siku ya kupiga kura ili CCM ipate ushindi wa kihistoria na kuendelea kushika Dola.
Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM Taifa,Mohammed Ali Kawaida amesema Kauli ya Mitano Tena ni kwa ajili ya viongozi wawili tu ndani ya CCM ambao ni Mwenyekiti wa CCM Taifa,Ndugu Samia Suluhu Hassan na Makamu wa Mwenyekiti CCM Zanzibar, Ndugu Hussein Ali Mwinyi.
No comments:
Post a Comment