Habari za Punde

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrisa Kitwana Mustafa, alipowasili katika viwanja vya Soko la Jumbi Wilaya ya Magharibi “B” Unguja, akiwa katika ziara yake kutembelea soko la jumbi kuangalia mwenendo wa biashara na upatikanaji wa bidhaa katika masoko ya Jumbi,Mwanakwerekwe na Darajani, ziara hiyo iliyofanyika leo 24-2-2025
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, akimsikiliza Mfanyabiashara wa mbogamboga katika Soko la Jumbi Wilaya ya Magharibi “B” Unguja, wakati wa ziara yake kutembelea Soko hilo kuangalia mwenendo wa biashara na upatikanaji wa bidhaa mbalimbali katika Soko hilo, ziara hiyo iliyofanyika leo 24-2-2025, na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrisa Kitwana Mustafa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, akiuliza swali kwa Mfanyabiashara wa mchele Stella Job, katika Soko la Jumbi Wilaya ya Magharibi “B”Unguja, wakati wa ziara yake kutembelea masoko ya Mkoa wa Mjini Magharibi leo 24-2-2025, Soko la Jumbi,Mwanakwerekwe na Darajani
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, akiangalia bidhaa ya mchele wakati wa ziara yake katika Soko la Jumbi Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 24-2-2025, kuangalia mwenendo wa biashara na upatikanaji wa bidhaa katika soko hilo




RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Wafanyabiashara wa Soko la Jumbi Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 24-2-2025, akiwa katika ziara yake katika masoko ya Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, kuangalia mwenendo wa biashara na upatikanaji wa bidhaa katika masoko hayo ya Jumbi,Mwanakwerekwe na Darajani

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.