Wafanyabiashara wa Kijiji cha Ipunga wametakiwa kufanya shughuli za kujitafutia kipato kwaajili ya familia zao bila kusahau malezi ya watoto wao ili kuwawezesha watoto kukua vizuri kutokana na uangalizi wao.
Hayo yamesemwa Juni 02, 2025 na Polisi Kata ya Ipunga, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Eletisia Mtweve alipokutana na wafanyabiashara wadogo wadogo katika Soko la Nakonde lililopo kata ya Ipunga Wilaya ya Mbozi Juni 02, 2025.
"Mnatakiwa kuwa karibu na watoto wenu ili wapate malezi bora ambayo yatajenga upendo na urafiki baina yenu na watoto ikiwa ni pamoja na kumfanya akupe taarifa ya vitendo vya ukatili anavyokumbana navyo akiwa shuleni na kwenye michezo yake ya kila siku" alisema Mkaguzi Eletisia.
Aidha, Mkaguzi Eletisia aliwataka wafanyabiashara hao kuacha mazoea ya kuwaacha watoto wao kwa majirani au kwa ndugu zao ili waende kwenye shughuli za utafitaju, jambo ambalo limepelekea kutokea kwa vitendo vya ukatili na unyanyasaji dhidi ya.watoto hao.
Jeshi la Polisi limeendelea kutoa elimu na kuyafikia makundi mbalimbali katika jamii ili kuwajengea uelewa kuhusu masuala ya usalama ikiwa ni pamoja na madhara ya uhalifu katika jamii.
No comments:
Post a Comment