Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi Amejumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika Sala ya Eid Al-Adha Iliyofanyika Masjid Taqwaa Bambi Mkoa wa Kusini Unguja

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwasili katika viwanja vya Masjid Taqwaa Bambi Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja kwa ajili ya Sala ya Eid Al-Adha, iliyofanyika katika masjid hiyo leo 7-6-2025, akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe.Ayoub Mohamed Mahmoud (kulia kwa Rais) na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Alhajj Dkt.Haroun Ali Suleiman
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Viongozi mbalimbali wa Serikali na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika Sala ya Eid Al-Adha, iliyofanyika leo 7-6-2025 katika Masjid Taqwaa Bambi Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali na Dini ya Kiislamu akifuatilia Hutuba ya Sala ya Eid Al-Adha, ikisomwa na Sheikh Abdurahaman Ahmed Abdallah, baada ya kumalizika kwa Sala ya Eid, iliyofanyika katika Masjid Taqwaa Bambi Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja iliyofanyika leo 7-6-2025.
WAUMINI wa Dini ya Kiislamu Zanzibar wakifuatilia hutuba ya Sala ya Eid Al-Adha ikisomwa na Sheikh Abdulrahaman Ahmed Abdallah, baada ya kumalizika kwa Sala ya Eid iliyofanyika katika Masjid Taqwaa Bambi Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja leo 7-6-2025
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijuika na Viongozi mbalimbali wa Serikali na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika kuitikia dua ikisomwa na Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Hassan Othman Ngwali (hayupo pichani) na (kushoto kwa Rais) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi, baada ya kumalizika kwa Sala ya Eid Al-Adha iliyofanyika katika Masjid Taqwaa Bambi Wilaya Kati.Mkoa wa Kusini Unguja leo 7-6-2025



RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na kuagana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Alhajj Othman Masoud Othman na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla, baada ya kumalizika kwa Sala ya Eid Al-Adha iliyofanyika katika Masjid Taqwaa Bambi Wilaya ya Kati,Mkoa wa Kusini Unguja leo 7-6-2025
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akifurahia jambo wakati akibadilishama mawazo na Viongozi wa Serikali,baada ya kumalizika kwa Sala ya Eid Al-Adha, iliyofanyika katika Masjid Taqwaa Bambi Wilaya ya Kati,Mkoa wa Kusini Unguja, iliyofanyika leo 7-6-2025. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.