Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis wakati akijibu maswali bungeni jijini
Dodoma leo tarehe 9 Juni 2025.
Hayo yamesemwa na
Naibu wa Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis
Hamza Khamis wakati akijibu swali la Mbunge wa Kilwa Kusini Mhe. Ally Kassinge aliyeuliza Serikali
ina mpango gani wa kujenga ukuta eneo la Pwani ya Mji wa Kilwa Kivinje ili
kuzuia maji ya Bahari yanayoathiri wananchi.
Mhe. Khamis ametaja hatua hizo kuwa ni
pamoja na kuendelea kufanya tathmini ya uharibifu wa fukwe zote katika ukanda
wa pwani, kuendelea kutenga na kutafuta fedha kupitia Mifuko ya Usimamizi wa
Mazingira na Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi ikiwemo, Mfuko wa Kuhimili
Mabadiliko ya Tabianchi (Adaptation Fund), GEF na GCF na Washirika wa Maendeleo
ikiwemo Benki ya Dunia.
Kwa muktadha huo Naibu Waziri Khamis alisisitiza kuwa shughuli
za ujenzi wa ukuta katika eneo hilo la pwani zitaanza kutekelezwa baada ya
fedha kupatikana.
Halikadhalika, alihimiza uongozi na
wananchi wa Kilwa Kivinje kuendelea kuongeza
jitihada za kutunza mazingira ya maeneo ya ufukwe kwa kudhibiti shughuli
zisizoendelevu za kibinadamu kwa kuongeza jitihada za kuhifadhi mazingira
na
upandaji wa miti kama ilivyobainishwa kwenye Sheria ya Usimamizi wa Mazingira.
Katika
hatua nyingine Mhe. Khamis alisema mradi wa ujenzi wa ukuta na matuta unaotekelezwa kwenye maeneo ya fukwe
za bahari ya hindi eneo la Sipwese Mkoa wa Kusini Pemba umefikia asilimia 99.
Alibainisha
hayo wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Asya
Mwadini Mohammed aliyetaka kujua kauli ya Serikali kuhusu ujenzi wa mradi huo
utakamilika lini ili kuwanusuru wananchi kwa changamoto ya kuingiliwa na maji
ya bahari.
Akiendelea
kujibu swali hilo, Naibu Waziri Khamis kutokana na kufikia hatua hiyo Serikali
kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais inatarajia kukabidhi mradi huo kwa wananchi
hivi karibuni.
Pia,
Naibu Waziri aliwasihi wananchi kuendelea kupanda miti hasa aina ya mikoko na
kuacha kuacha kukata miti pamoja na kufanya shughuli zinazoharibu mazingira.
Alitoa
rai hiyo wakati akijibu swali la Mbunge wa Amani Mhe. Abdul Yussuf Maalimu
aliyetaka kujua Serikali ina mpango gani wa kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira
hasa kwenye maeneo ya bahari yanayotumika katika shughuli za uchumi wa buluu.
“Uchumi
wa buluu ni pamoja na shughuli mbalimbali ndani ya bahari zikiwemo uvuvi, ulimaji
wa mwani na masuala ya utafiti wa kwa ajili ya ugunduzi wa mafuta na gesi,
kwahiyo shughuli hizi zimekuwa zikiharibu mazingira kwa namna ama nyingine kwa
kiasi fulani, mheshimiwa tumechukua hatua mbalimbali zikiwemo kutoa elimu kwa
wananchi,” alisisitiza.
No comments:
Post a Comment