Na.Mwandishi Afya Zanzibar
WIZARA ya Afya
Zanzibar imesema imejipanga katika kukabiliana na magonjwa mbali mbali kwa
wananchi, wageni na wanamichezo watakaoshiriki katika mashindano ya CHAN
yanayotarajiwa kufanyika mapema mwezi uajao katika visiwa vya Zanzibar.
Akizungumza mara
baada ya kufanya ziara maalumu katika Hospitali ya Mkoa wa Mjini Magharibi
Lumumba ambayo ni miongoni mwa Hospitali itakayotumika kutoa huduma wakati wa
mashindano ya CAHAN, Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Hassan Khamis Hafidh amesema Wizara ya Afya Zanzibar imejipanga
katika kuahakikisha kuwa usalama wa kiafya kwa wageni na wenyeji katika mashidano hayo yanakuwa na ubora wa
hali ya juu.
Amesema ni fursa
ya kipekee kwa nchi ya Zanzibar kuwa mwenyeji wa mashindano hayo na kufanikisha
kwa maendeleo makubwa yanaletwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika
suala zima la kuimarisha michezo hapa nchini.
Amefahamisha
kuwa katika kukabiliana na hali ya kiafya katika kipindi chote cha mashindano
ya CHAN Wizara ya Afya imejipanga kwa kuwa na Madaktari wa kutosha, vifaa tiba,
usafiri wa dharura pamoja na dawa zote muhimu katika Hospitali ya Lumumba.
Kwa upande wake
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dkt Mngereza Mzee Miraji amesema lengo la
ziara hiyo ni kuangalia maandalizi ya afya katika kipindi chote cha mashindano
ya CHAN yanayotarajiwa kufanyika hivi karibuni hapa nchini.
Aidha amesema katika
kufanikisha mashindano hayo Wizara ya Afya imeandaa mikakati madhubuti ya
kuhakikisha wageni na wenyeji na wanamichezo wanakuwa salama na magonjwa na
mashindano hayo yanafanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Afisa tabibu Mkuu wa Hospitali ya Lumumba Dkt, Yasser El Bahy, amesema Hospitali hiyo ipo tayari kutoa huduma wakati wote kwa wageni na wananchi na kusisitiza kuwa vifaa, Dawa zipo za kutosha katika kukabiliana na hali yoyote.
Ziara hiyo imewashirikisha kamati ya Afya ya CHAN kutoka Wizara ya Afya na imehusisha maeneo tofauti ikiwemo, Hoteli za Kulaza wageni, uwanja wa New Amani Complex, Hospitali ya Mkoa Lumumba ikiwa na lengo la kuhakikisha kuwa maandalizi ya kiafya yanakwenda sambamba na viwango vinavyohitajika katika mashindano hayo.
Katika hatua nyengine Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Hassan Khamis Hafidh ameitaka kamati ya afya inayoshughulikia maandalizi ya CHAN kukabilina na changamoto na kuimarisha mipango na utekelezaji majukumu yao.
Ameyaeleza hayo katika kikao maalum kwa wanakamati wa afya huko Wizara ya Afya ambacho kimelenga hatua zilizofikiwa katika maandalizi ya afya kwa ajili mashindano ya CHAN pamoja na kujadili namna kuongeza nguvu katika maeneo yenye changamoto ili kuyaimarisha zaidi.
Mwisho
No comments:
Post a Comment