Habari za Punde

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Awasili Nchini Belarus kwa Ziara ya Kikazi ya Siku Tatu

 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Waziri Mkuu wa Beralus,  Viktor Karankevich alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Minsk nchini  Belarus  kuanza  ziara ya kikazi ya siku tatu nchini humo, Julai 21, 2025.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akichukuwa kipande cha mkate ukiwa ni utamaduni wa kukaribisha wageni nchini Belarus alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Minsk nchini humo kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu, Julai 21, 2025.

Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa  na Mkewe  Mary Majaliwa wakipewa  maua walipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Minsk nchini Belarus kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu nchini humo, Julai 21, 2025.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Waziri Mkuu wa Belarus, Viktor  Karankevich alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Minsk nchini Belarus kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu nchini humo, Julai 21, 2025. Wengine kutoka kushoto ni Balozi wa Tanzania Urusi na Belarusi, Frederick Ibrahim Kibuta ,  Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais, Kazi , Uchumi na Uwekezaji Zanzibar, Shariff Ali Shariff, na watatu kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Cosato Chumi. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Waziri Mkuu wa Belarus, Viktor  Karankevich alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Minsk nchini Belarus kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu nchini humo, Julai 21, 2025.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.