Habari za Punde

WAZIRI MKUU AKAGUA MAANDALIZI YA KILELE CHA MBIO ZA MWENGE WA UHURU NA KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE

 

Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza alipokagua  Maandalizi ya Kilele cha  Mbio za Mwenge wa Uhuru na Kumbukizi ya Baba wa Taifa kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya Oktoba 13, 2025. Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, William Lukuvi  (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Benno Malisa alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Songwe na baadae alikagua  Maandalizi ya Kilele cha  Mbio za Mwenge wa Uhuru na Kumbukizi ya Baba wa Taifa kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya Oktoba 13, 2025.  Pia alitoa tamko katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupunguza Madhara ya Maafa kwenye ukumbi wa City Park Garden jijini Mbeya.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete wakati alipokagua  Maandalizi ya Kilele cha  Mbio za Mwenge wa Uhuru na Kumbukizi ya Baba wa Taifa kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.




Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza alipotoa tamko katika Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Kupunguza Madhara ya Maafa kwenye ukumbi wa City Park Garden jijini Mbeya, Oktoba 13, 2025.
Baadhi ya viongozi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipozungumza baada ya kukagua  Maandalizi ya Kilele cha  Mbio za Mwenge wa Uhuru na Kumbukizi ya Baba wa Taifa kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya Oktoba 13, 2025.

Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.