SMZ kununua mashine ya DNA
NAIBU Waziri wa Afya, Dk. Sira Ubwa Mamboya, amesema Serikali ina mpango wa kununua mashine ya DNA kutokana na umuhimu wake.
Alisema mpaka sasa Serikali imeshafanya upembuzi yakinifu kwa kushirikiana na ofisi ya maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ya Muungano, pamoja na kutayarisha jengo la Mkemia Mkuu kwa ajili ya kuweka mashine hiyo.
Dk. Sira alisema hayo katika kikao cha Baraza la Wawakilishi alipokuwa akijibu suali la Fatma Mabrouk Said (Amani), aliyetaka kufahamu Serikali ina mpango gani wa kupatikana kipimo hicho hapa nchini.
Aidha alisema DNA ni mashine ya kupima uasilia pale panapotokezea utata wa mtoto, kipimo hicho hufanyika baada ya kuzaliwa mtoto na kuthibitisha nani baba halisi.
Sambamba na hayo alisema suala la kuwapa mimba wasichana ni ukosefu wa maadili na hakuna uhusiano na ukosefu wa mashine hiyo.
MEYA KIBAHA KUTOA ZAIDI YA MILION 18 KUCHIMBA VISIMA VINNE KUPUNGUZA KERO
YA MAJI PANGANI
-
Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha Disemba 22, 2025
Baadhi ya wananchi wa Mtaa wa Kidimu, Kata ya Pangani, Halmashauri ya
Manispaa ya Kibaha wanakabiliwa na uhaba...
11 hours ago
0 Comments