6/recent/ticker-posts

MUFTI ATAKA MADUNGU WAUNDE POLISI JAMII

Na Suleiman Rashid, Pemba

MUFTI Mkuu wa Zanzibar Sheikh Salehe Omar Qaabi, amewataka wananchi wa Madungu mtaa wa majumba makubwa kuanzisha kamati ya Polisi jamii katika shehia hiyo kwa lengo la kupambana na vitendo viovu vilivyokithiri katika eneo hilo.

Mufti Qaabi alieleza hayo alipofanya mazungumzo ya pamoja na wakaazi wa eneo hilo ambapo pamoja na mambo mengine, wananchi hao walimpongeza kufuatia hivi karibuni kuteuliwa kuwa Mufti Mkuu wa Zanzibar.


Katika nasaha zake Mufti huyo aliwataka wananchi wa Madungu majumba makubwa kuhakikisha wanaunda polisi jamii hali itakayowawezesha kuvidhibiti vitendo viovu.

Aidha alisema kuwa siri ya mafaniko katika jamii ni ushirikiano huku akiwaomba wananchi hao kuendeleza umoja miongoni mwao kwa kujilinda na maovu na majanga ya kidunia kwa kuwa na kikindi kitakacho shirikiana na vyombo venye nguvu ya kushinda lengo na azma ya wale wanaotekeleza maovu katika jamiii.

Akizungumzia kuhusu malezi ya watoto, Sheikh Qaabi alisema aliwasihi wazee kuwajengea itikadi watoto wao na vijana hao ili kupata watu wenye maadili na kuwataka wazee kuhakikisha watoto wao wanajipatia elimu ya dunia na ile ya akhera.

“Nakusihini kuendeleza umoja na mashirikiano,kama uliopo ili tujenge maadili mema yetu tulionayo watu Zanzibar”, alisema Mufti Qaabi.

Kabla ya kuteuliwa kuwa Mufti wa Zanzibar, Sheikh Qaabi alikuwa mlezi mwelekezi wa kamati katika shehia ya Madungu mtaa wa majumba marefu kwa muda wa miaka minne.

Mapema akitoa shukurani zake kwa niaba ya kamati hiyo Mwenyekiti wa kamati hiyo Abrahamani Makame Shafi aliahidi kufata nyayo na maelekezo aliyowaachia Mufti huyo.

Wanakamati hao waliomba dua ya pamoja kumuombea kheri na fanaka wakati huu wa kukabiliana na nafasi hio kubwa na mzito ya kuwa mufti mkuu wa Zanzibar na kumpongeza Rais wa Zanzibar kuwateulia mtu aliekuwa kwenye kamati yao.

Kamati hio hiyo ya Madungu jumba namba nne iliyoanzishwa miaka minne iliyopita ilikuendeleza shughuli za usafi wa jumba lao na kusimamia malezi ya watoto.

Post a Comment

0 Comments