6/recent/ticker-posts

WATOTO WENGI KUPATIWA CHANJO MWAKA HUU

Dk. Shein kuongoza kampeni Mwambe Pemba

Na Juma Masoud

ZIKIWA zimesalia takriban siku sita kabla ya uzinduzi rasmi wa zoezi la chanjo kitaifa litakalofanyika Mwambe Kusini Pemba, maandalizi kamili ya zoezi hilo yamekamilika.

Mkuu wa kitengo cha Afya katika Wizara ya Afya, Abdulrahman Mussa Kwaza amewaambia waandishi wa habarti mjini hapa mwishoni mwa wiki kwamba uzinduzi huo utafanywa na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein Jumamosi ijayo na kuendelea kwa siku tatu hadi Jumatatu ya Novemba 14.


Kwa mujibu wa ofisa huyo vituo 440 vimetayarishwa kwa ajili ya zoezi hilo, ambalo litakwenda sambamba kwa siku zote tatu Unguja na Pemba, huku vingi ya vituo vitakavyotumika kwa zoezi hilo ni vituo vya afya.

Chanjo zitakazotolewa katika zoezi hilo ni shurua, kwa watoto kuanzia miezi tisa hadi miaka mitano, chanjo ya Polio itawahusisha watoto kuanzia kuzaliwa hadi miaka mitano na utoaji wa Vitamin ‘A’ ni kwa ajili ya watoto wenye umri kuanzia miezi sita hadi miaka mitano.

Aidha, utoaji wa dawa ya minyoo utawahusisha watoto wenye umri kuanzia mwaka mmoja hadi miaka mitano.

Kulingana na ofisa huyo, zoezi la chanjo la mwaka huu pia litahusisha mpango wa kupima ukuaji wa mtoto ambapo kipimo maalu kitatumika kujua ukuaji wa mtoto kama uko katika hali nzuri, ya kawaida ama hali mbaya ambapo mtoto wa aina hiyo ataweza kupatiwa uangalizi wa ziada.

Habari ambazo gazeti hili imezipata zinaonesha kwamba zaidi ya watoto 658,024 wenye umri wa kuanzia siku moja hadi miaka mitano watahusika na zoezi hilo.

Wanaotarajiwa kupatiwa chanjo ya surua ni 198,833, Polio wastani ni watoto, 237,472, vitamin ‘A’ wastani ni watoto 211, 719, ingawa takwimu za wanaopatiwa dawa ya hazikupatikana.

Wazi na walezi watoto wenye umri kuanzia siku moja hadi miaka mitano wanahimizwa kuwafikisha watoto kwenye vituo husika ili wapatiwe chanjo hiyo muhimu.

Aidha, wazazi wamekumbushwa kuwa hawawajibiki kuchukua magamba ya watoto wao wala karatasi za kuzaliwa.

Chanjo ya mwisho kitaifa ilifanyika Uroa, Mkoa wa Kusini Unguja mwaka 2008.

Post a Comment

0 Comments