6/recent/ticker-posts

BREAKING NEWS........ALIYEKUWA MPIGA PICHA WA MARAIS WA AWAMU YA TANO NA SITA MWINYIMVUA AHMED ALI AMEFARIKI MCHANA WA LEO ZENJ

MPIGAPICHA mwandamizi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar, Mwinyimvua Ahmed Ali amefariki dunia jana katika Hospitali kuu ya Mnazi Mmoja mjini Zanzibar, alikokua amelazwa kwa muda.

Kwa mujibu wa taarifa ilioyolewa kwa vyombo vya habari na Idara ya Habari Melezo imeeleza kua marehemu huyo kabla ya kifo chake, alikua akisumbuliwa na ungonjwa wa sindikizo la damu ambapo tokea juzi alikuwa amelazwa katika chumba mahatuti kwa uangalifu  maalum wa daktari .

“Mwinyimvua kabla ya kifo chake tokea juzi alikua amezidiwa sana na kulazimika kuhamishiwa chIumba maalum (ICU) kwa ajili ya uangalizi wa daktari ambapo jana hali ikawa mbaya na kufariki dunia’’,lieleza taarifa hiyo.


Taarifa hiyo imezidi kueleza kua marehemu huyo mwenye umri wa miaka 56, aliajiriwa na Idara ya Habari na Utangaazaji wakati huo ,akiwa na umri wa miaka 18 akiwa mpiga picha, na baadae kupata mafunzo ya upigaji wa picha nchini Japan kwa muda wa mwaka mmoja.

Mwinyimvua aliporudi masomoni alihamishiwa Ikulu na kua mpiga mpicha wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mpinduiz wakati huo Dk Salmin Amour Juma , na baadae Rais wa awamu ya sita Dk Aman Abeid Karume.

Katika uhai wake marehemu alifanya kazi hiyo Ikulu ya Zanzibar kwa muda wa miaka 20 mfululizo, ambapo mwaka jana, (2011) alirejeshwa tena Idara ya Habara Maelezo, na kua mpiga mpicha mwandamizi .

Marehemu huyo anatarajiwa kuzikwa leo mchana kijijini kwao Fuoni kesho mchana na amewacha watoto watano na mke mmoja

Mwaka uliomalizika jumla ya waandishi wa habari kadhaa wa Zanzibar akiwemo Maulid Hamad Maulid , Bakar Sauti Mirando, na Halima Mchuka na John Ngayoma kwa Tanzania bara walifarikia dunia ambapo na mwaka huu tasnia ya habari imeondokea na mpiga picha mwandamizi Mwinyimvua Ahmed Ali

Post a Comment

2 Comments

  1. Inna Lil-lahi Wa inna ilaihi Raji-uun. M/mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi.. amin.

    ReplyDelete
  2. Innalillahi waina illayhil rajiuna. munguy akupe kauli na akulaze mahala pema peponi inshaalah.

    Makame Hj Mohamed.

    KL - my

    ReplyDelete