6/recent/ticker-posts

Waziri alipongeza shirika la Bima

Na Juma Mmanga, ARUSHA
WAZIRI wa Nchi Fedha Uchumi na Mipango ya Maendeleo, Omar Yussuf Mzee amelipongeza shirika la Bima la Zanzibar kutokana na kufanyakazi kwa ufanisi.

Waziri huyo alieleza hayo Arusha hivi, alipokuwa akifungua semina elekezi kwa mawakala wa shirika hilo kanda ya kaskazini mwa Tanzania.

Alisema shirika hilo linastahili sifa kutokana na kujitanua kwake kibiashara hali iliyolifanya kukubalika kwa wananchi wa Zanzibar na kila sehemu inapotoa huduma zake Tanzania bara.

“Serikali ya Mapinduzi inajivunia kazi nzuri inayofanywa na shirika hili, endeleeni kutekeleza majukumu yenu na ufanisi zaidi utapatikana”, alisema waziri huyo.

Aliwaeleza mawalaka hao kujituma zaidi katika kutekeleza majukumu yao na kwamba shirika hilo kujikita kufanyabishara Tanzania bara ni miongoni mwa matunda ya Muungano.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo Abdul Nassir Ahmed alisema shirika lake limeona umuhimu wa kuwapatia mafunzo mawakala hao ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

“Mawakala ndio nguzo yetu muhimu kwenye biashara ya bima, tumefanya mafunzo haya ili kuhakikisha wanatekeleza kwa ufanisi makujumu yao”,alisema Mkurugenzi huyo.

Semina hiyo pia iliwashirikisha baadhi ya wenyeviti wa kamati za kudumu Baraza la Wawakilishi, ambao nao hawakusita kulipongeza shirika hilo.



Post a Comment

1 Comments

  1. Hata miminalipongeza shirika hili pamoja nayale yote yaliyofanikiwa kuvuka mipaka ya Z'bar.

    Taasi kama PBZ, Bima na Z'ntel naona wamejitahidi, na wanafaa kupongezwa.

    Changamoto inabaki kwa mashirika kama ZBC waige mfano wao.

    ReplyDelete