6/recent/ticker-posts

Dk Bilal atembelea kituo cha mafunzo ya Kompyuta Chwaka

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Viongozi wa Kituo cha Mafunzo ya Kompyuta cha Chwaka na wananchi wa kijiji hicho, wakati alipofika katika kituo hicho leo Desemba 24, 2012 kwa ajili ya kujionea maendeleo ya kituo hicho, akiwa ameongozana na mkewe Mama Asha Bilal. 
Sehemu ya Kompyuta zilizopo katika Kituo hicho cha mafunzo ya Kompyuta cha Chwaka
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Mjumbe wa
Kamati ya Maendeleo ya Kijiji cha Chwaka, Hamis Himid Ramadhan, wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya Kituo cha mafunzo ya Kompyuta cha Chwaka (CCTC) leo Desemba 24, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Asha Bilal, wakiondoka katika Kituo cha mafunzo ya Kompyuta cha Chwaka (CCTC) baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya kituo hicho leo, Desemba 24, 2012. Picha na OMR

Post a Comment

0 Comments