Wadada wakali wa Epiq BSS
waliofanikiwa kuingia TOP 10, Nsami Nkwabi, Husna Nassor na Menina Atik, wamewapa
mashabiki wao zawadi ya nyimbo mpya kwa ajili ya sikukuu ya Christmass.
Wadada hao ambao walitoa burudani ya
kutosha wakati wa mashindano hayo, hivyo kujijengea mashabiki kibao, Husna
akiwa kajikita kwenye miziki ya Taarab, na Nsami na Menina wakiimba miziki
laini, wamesema zawadi hiyo ni maalumu kwa mashabiki wao kwa ajili ya Christmass.
Nsami, ambaye alishika nafasi ya nne,
wimbo wake unaitwa ‘NILIDHANI’, ambao kaufanyia studio ya Surround Sounds chini
ya mtayarishaji EMA the Boy, na umendikwa na mkali kutoka THT, Amini.
Akiuzungumzia wimbo huo, Nsami
anasema ameufanya wimbo huo mapema ili kuonyesha uwezo wake, na anaamini
utawashika wapenda burudani nchini.
‘Wimbo huu unamuonyesha Nsami, ambaye
wengi wenu mlipigia kura wakati wa mashindano, hivyo ninaomba muendelee
kunisapoti kwa zangu nyingi zinazokuja’ anasema Nsami.
Kwa upande wake yule mshiriki
aliyeingia kwa Wild Card, Menina, yeye wimbo wake unaitwa ‘DREAM TONIGHT’ ,
ambao ameufanya chini ya Studio ya Surround Sound, mtayarishaji akiwa EMA the
Boy na mtunzi akiwa Nash Designer.
‘Dream tonight ni wimbo ambao hakika
utawafanya watanzania wamjue Menina hasa, kwani ni wimbo ambao ni wa kiburudani
zaidi tofauti na wengi walivyonizoea nikiwa katika Epiq BSS’ anasema Menina.
Mshiriki Husna, ambaye alijijengea
jina kwa kuimba nyimbo za Taarab, ameendeleza ukali wake kwa kutoa kibao chake
cha mduara, ‘NAWAMIMINA’ kikiwa kimetayarishwa na EMA the Boy na kuandikwa na
Nash Designer.
‘Nimeamua kuendelea kuwapa burudani
ambayo wengi wenu mliizoea toka kwenye mashindano ya BSS, lakini nina uhakika
wimbo huu utaleta mabadiliko kwenye soko la muziki wa Taarab hapa nchini’
anasema Husna.
Nyimbo hizo zinatoka zikufuatia wimbo wa Wababa
Mtuka, mshindi namba tatu wa Epiq BSS uliotoka wiki iliyopita unaoitwa, My
Wife,ambao unafanya vizuri kwenye radio zote hapa nchini
0 Comments