Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, kwa mujibu wa uwezo aliopewa Chini ya Kifungu cha 119 (1) cha Katiba ya Zanzibar ya 1984, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein, amemteua Bw. Jecha Salim Jecha kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar.Aidha amewachagua wafuato kuwa Wajumbe wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar.
1 -- Balozi Omar Ramadhani Mapuri -- Mjumbe
2-- Bw. Salmin Senga Salmin -- Mjumbe
3 -- Bw. Nassor Khamis Mohammed -- Mjumbe
4 -- Bw. Ayuob Bakari Hamad --- Mjumbe
5 -- Jaji . Abdulhakim Ameir Issa --- Mjumbe
6 --- Bw. Haji Ramadhan Haji --- Mjumbe
Uteuzi huo umeanza leo tarehe 30 Aprili 2013
Pia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, amemteuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja
Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 61 (1) cha Katiba ya Zanzibar ya 1984, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein, amemteuwa Dkt. Idris Muslim Hija kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja.
Uteuzi huo umeaza leo 30-4-2013
Viongozi hao wanatarajiwa kuapishwa siku ya jumamosi 4-5-2013, saa 2.30 Ikulu ya Zanzibar.
5 Comments
hili ni tatizo , ikiwa rais atateua hawa watu wa tume ya uchaguzi , unategemea nini? si watampendelea katika masuala ya uchaguzi. Hili jukumu lazima liondoshwe kwa rais , lipelekwe kwa wananchi kupitia baraza la wawakilishi kuchagua wajumbe, na baadae miongoni mwa wajumbe wachague mwenyekiti wao,
ReplyDeleteKuhusu Uteuzi wa Tume ya Uchaguzi, kwani Raais haoni kuna wanawake pia waliosoma ambao wanafaa kuteuliwa. Hakuna hata mmoja hapa.
ReplyDeleteNchi hii viongozi huwa hawastaafu..yaani wale wale Bin kinanat, Bin mudriqat wa Bin Illyas!
ReplyDeleteNapata tabu kujua, haya ni matatizo ya muungano au yetu wenyewe!
Ndugu yangu kunabaazi ya vyama vilipewa barua yakupeleka majina ya wwajumbe wanao taka sasa ilkuwa wapeleke hayo majina ya wanaake walosoma
ReplyDeleteTuliwaondoa bunkina weupe sasa tupo sisi weusi tutalindana mpaka na sisi tupinduliwe
ReplyDelete