Jumla ya Shilingi milioni 16 zinahitajika ili kufanikisha safari ya Sheikh Azzan Khalid Hamdan kuelekea nchini India kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Sheikh Azzan amesema milango iko wazi kwa yeyote mwenye uwezo kumsaidia kufanikisha safari yake kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Sheikh Azzan amesema yeyote mwenye mchango wake anaweza kuutuma kupitia akaunti yake ya tigo pesa 0715434145 iliyosajiliwa kwa jina lake ama kwa anayetaka kufanya mawasiliano ya moja kwa moja anaweza kumpata kupitia 0777434145.
Aidha amesema michango hiyo inaweza kutumwa kupitia akaunti namba 0112055369500 Benki ya CRDB tawi la Zanzibar AZAN KHALID HAMDAN.
Sheikh Azzan amesema safari yake itafanyika mara baada ya kukamilika kwa taratibu ikiwemo gharama za matibabu na usafiri baada ya kupatiwa dhamana ya matibabu nje ya nchi.
Taarifa na Munir Zakaria
0 Comments