Utekelezaji wa sheria, uadilifu na kujituma kwa bidii
Na Bakar Mussa - Beijing, China .
Utekelezaji
wa Sheria za Nchi, Uadilifu na kujituma
kwa bidii kwa Wananchi na Viongozi wa China ndio siri kubwa ya mafanikio
ya Kimaendeleo Nchini humo.
Hayo yalielezwa na Profesa , Liu Juinjie,
kutoka Skuli ya Chama cha Kikomunisti cha China huko katika Hoteli ya Yongan
, Mjini Beijing China ,
wakati alipokuwa akiwasilisha mada ya Mfumo wa Kisiasa nchini humo na Uzoefu wa
Wananchi katika kujiletea maendeleo yao .
Alisema kuwa kumekuwepo Utii wa Sheria bila
ya kuwepo mtu aliejuu ya Sheria za Nchi , kumepelekea nchi hiyo kupiga hatuwa kubwa ya Kimaendeleo
ya Uchumi na Viwanda na kuwa miongoni mwa Mataifa tajiri Duniani.
“ Hakuna
mtu aliejuu ya Sheria katika Nchi yetu ya China , hususana katika suala la
kujiletea maendeleo na ndio nchi yetu tukawa tunapambana na Vitendo viovu
vinavyo rejesha nyuma maendeleo yetu ikiwemo Rushwa “ alisema Profisa, Liu.
Profesa Liu Junjie alifahamisha kuwa
kutokana na usawa huo mbele ya Sheria za nchi uliopo China , ndio Wananchi wake
wanashikamana pamoja na kuwa bega kwa bega na Viongozi wao wa Serikali katika
harakati za maendeleo chini ya Mfumo wa Chama Kimoja cha Kikomunisti
“ Mfumo wetu wa Chama kimoja tunaoendelea nao ni mzuri
na unatufaa nchini kwetu kwa vile hatuna migogoro katika Uongozi wa Nchi , kwa
vile Wananchi wetu na Viongozi wao daima wanashikamana lengo likiwa ni
maendeleo mbele,” alieleza Profesa huyo.
Alisema kuwa Nchi ya China ambayo kwa sasa
inakisiwa kuwa na zaidi ya Watu 1.3 Bilion,i itaendelea kuwa nchi ya Kimaendeleo
kwa vile bado wanamkubuka Wasia wa Muasisi wa Chama hicho cha Kikomunisti ,
Hayati Mao Dztung, ambaye aliiwezesha Nchi hiyo kuwa na
maendeleo ya haraka.
Hivyo alifahamisha kuwa China imekuwa
ikipiga hatuwa kubwa ya Kimaendeleo siku hadi siku na kuleta mabadiliko ya
kweli na haraka tafauti na nchi nyingi Duniani na kuiwezesha kuwa na marafiki
wengi ambao wanasaidiana nao katika mambo mbali ya Kimaendeleo ya kila Sekta.
0 Comments