Mshiriki Joshua Kahoza
akiimba wakati wa mkutano na waandishi wa habari. Anayetazama kushoto ni
Mtaalamu wa Huduma za Ziada wa Zantel, Cecil Muhina, na jaji mkuu wa Epiq BSS,
Ritha Paulsen.
Jaji Mkuu wa Epiq BSS,
Ritha Paulsen, akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusiana na maenedeleo
ya kipindi hicho. Kulia kwake ni Haji Yussuf, Meneja Huduma za ziada, na
kushoto ni Mtaalamu wa huduma za ziada, Cecil Muhina.
Mshiriki First Godfrey akiimba mbele ya waandishi wa habari. Anayetazama kushoto ni Mtaalamu wa Huduma za Ziada wa Zantel, Cecil Muhina, na jaji mkuu wa Epiq BSS, Ritha Paulsen, mwisho ni Haji Yussuf, Meneja Huduma za Ziada
Mshiriki Elizabeth
Mwaakijambile akitoa burudani kwa waandishi wa habari leo. Anayetazama kushoto
ni Mtaalamu wa Huduma za Ziada wa Zantel, Cecil Muhina, na jaji mkuu wa Epiq
BSS, Ritha Paulsen.
Dar es Salaam, 7-10-2013: Shindano la
kuimba la Epiq BSS limeingia hatua za mwisho wiki hii likiwa limebakiza
washiriki kumi na mbili, kuelekea kumpata mshindi wa shilingi milioni hamsini
pamoja na mkataba wa kurekodi.
Washiriki waliochaguliwa kwa usaili
wa simu, nao waliungana na wenzao waliongia kumi bora wiki hii na konyesha
uwezo mkubwa, hali inayoashiria kutakuwa na kazi kubwa kumchagua mshindi.
Washiriki waliobaki mpaka sasa na
namba zao za ushiriki ni Amina Chibaba (03), Elizabeth
Mwakijambile (08), Emmanuel Msuya (21), First Godfrey (11), Francis Flavian
(09), Furaha Charles (14), Furaha Mkwama (06), Joshua Kahoza (02), Maina Thadei
(5), Mandela Nicholas (10), Melisa John (22) na Raymond John (23).
Akizungumzia hatua ambayo shindano
limefikia, jaji mkuu wa shidano hilo, Ritha Paulsen, aliwataka wananchi watumie
vema nafasi ya kupiga kura kwa kuchagua washiriki wenye vipaji vikubwa.
‘Hatua hii ni muhimu sana, hasa kwa
kuwa inalirudisha shindano kwa wananchi ili waweze kumchagua mshindi wao, hivyo
nawaomba wawapigie kura kwa wingi’ alisema Ritha.
Akizungumzia ubora wa washiriki wa
mwaka huu, Ritha alisema wamepata washiriki bora zaidi, na pia mafunzo
wanayoyapata ndani ya jumba la Epiq BSS ni makubwa hivyo mashabiki watarajie
mchuano mkubwa zaidi katika kuwania milioni hamsini.
Kwa upande wake Afsa Biashara Mkuu wa
Zantel, Sajid Khan, amewataka wananchi wawapigie kura washiriki wanaoamini ni
wazuri na watafanya vizuri kwenye soko.
‘Maana ya kufungua laini za watu
kupiga kura mapema ni kuwapa nafasi ya kuchagua mshindi wanayempenda’ alisema
Khan.
Kampuni ya Zantel
pia imerahisisha namna ya upigaji kura kwa kutoa namba maalumu ya kupiga kura
kwa kupiga simu namba 0901551000, na kwa njia ya ujumbe mfupi mashabiki wa Epiq
BSS wataweza kuwapigia washiriki wanaowapenda kwa kuandika neno KURA, halafu
waache nafasi, namba ya mshiriki halafu watume kwenda 15530.



0 Comments