Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete amewasili mjini Njombe jana, Alhamisi, Oktoba 17, 2013, kuanza
ziara ya wiki moja kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo katika Mkoa wa
Njombe.
Miongoni mwa shughuli kubwa ambazo Rais Kikwete
atazifanya katika ziara hiyo, ya kwake ya kwanza tokea Njombe kutangaza kuwa
Mkoa, ni kuuzindua rasmi Mkoa huo.
Katika siku yake ya kwanza kesho, Ijumaa, Oktoba 18,
2013, mbali na kuzindua Mkoa wa Njombe pia atazindua Kiwanda cha Chai katika
eneo la Ikanga na kuzungumza na wananchi.
Katika ziara hiyo ambako Rais Kikwete atatembelea
wilaya zote za mkoa huo ambazo ni Njombe, Wanging’ombe, Ludewa na Makete, pia
atazindua Chuo cha Veta cha Mkoa.
Aidha, Rais atatembelea na kupata taarifa kuhusu
maendeleo ya mradi wa chuma wa Liganga.
0 Comments