6/recent/ticker-posts

Utalii Mzuri Kaja

Utalii Mzuri kaja umelenga kupeleka wageni kwenye mashamba ya kilimo. Kwenye mashamba hayo masimulizi ya kilimo cha migomba kitaalamu na kienyeji hutolewa. Aidha hadithi za wazee zinazohusishwa na migomba pia hutolewa.
 
Kubwa zaidi watu wa Makunduchi kwa jumla wanatafuta njia ya kuuza ndizi zao  moja kwa moja kwa wafanyakazi maofisini kwa kutumia mtandao.
 
Njia hii itamsaidia mnunuzi kuchagua ndizi aipendayo ikiwa shambani wakati mnunuzi yuko afisini.  Makubaliano yakishafikiwa ndizi hiyo itawasilishwa kwa mwenyewe afisini alipo.

 Juhudi hizi za kutafuta kuuza ndizi kwa njia ya mtandao zinalenga kuondoa unyonyaji unaofanjwa na madalali kwenye Marikiti yetu ya Mpendae na Mwanakwerekwe.

Post a Comment

0 Comments