6/recent/ticker-posts

Wizara Yalaani Mauaji ya Mjamzito

Na Mwanajuma Mmanga
WIZARA ya Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto imelaani kitendo cha mauaji ya kikatili alichofanyiwa mama Mjamzito mkaazi wa Donge Mtambile Wilaya ya Kaskazini "B" Unguja ambayo yalisababishwa na mumewe.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi huko nyumba ya kulelea watoto Mazizini, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Msham Abdalla Khamis, alisema wamelipokea kwa masikitiko tukio hilo la kikatili dhidi ya mwanamke huyo.

Alisema mauaji hayo ya mwanamke ambae amefahamika kwa jina la Msikitu Juma Ali amefanyiwa vitendo vya kikatili ambavyo vinakiuka haki za binaadamu.

Aidha, alisema unyanyasaji wa kijinsia kwa wananwake na watoto wanaofanyiwa na wanaume limekuwa kubwa na na kuonekana kuwa ni la kawaida hapa nchini jambo ambalo linakiuka sheria na haki za binaadamu.

Alisema serikali kwa kushirikaina na Wizara ambayo inayosimamia masuala ya kama hayo wameamua kuandaa mipango mbalimbali ya kuelimisha jamii juu ubaya wa udhalilishaji na ukatili kwa wanawake na watoto.


Hivyo ameishauri jamii kuripoti mapema matukio kama hayo wakati wanapofanyiwa vitendo hivyo na muhalifu kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Alifahamisha kuwa jumla ya kesi saba zimeripotiwa katika kituo hicho kwa Unguja na Pemba ambapo kati ya hizo zimepatiwa ufumbuzi wa mahakamani kisiwani Pemba.

Hivyo, alisisitiza jamii kutoa ushirikiano na vyombo vya sheria katika kutoa ushahidi mahakamani kuhusiana na suala la udhalilishaji na ukatili wa kijinsia unaofanywa kila siku.

Marehemu huyo alipatwa na ajali hiyo wakati akiwa anaswali sala ya alfajiri ambapo alijeruhiwa kichwani na tumbo na kusababisha kifo chake.

Post a Comment

0 Comments