Makamu wa Kwanza wa Rais wa
Zanzibar Mhe.
Maalim Seif Sharif Hamad, akitembelea sehemu inayoingia maji ya chumvi katika
eneo la Kilimani mjini Zanzibar, kushoto Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni Mhe Mahmoud Mohammed Mussa.
Mkurugenzi
wa Idara ya Mazingira Zanzibar Sheha Mjaja Juma, akitoa maelezo mbele ya Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, kuhusiana na
kuingia maji ya chumvi katika
eneo la Kilimani mjini Zanzibar.
Afisa Tawala Mkoa wa Kaskazini Unguja Dr. Makame Ali Ussi, akitoa
maelezo mbele ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif
Hamad, kuhusiana na kuingia maji ya chumvi katika eneo la Fungu refu,
Mkokotoni. Wilaya ya Kaskazini Unguja
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akishuhudia hali ya uharibifu katika hoteli ya Zalu Nungwi, uliotokana na upepo mkali uliovuma katika Mkoa wa Kaskazini Unguja Jumapili usiku, na kusababisha majengo na maeneo kadhaa kuharibiwa vibaya.
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akitembelea skuli
ya Nungwi, kuangalia uharibifu uliotokana na upepo mkali uliovuma katika Mkoa
wa Kaskazini Unguja Jumapili usiku, na kusababisha majengo na maeneo kadhaa
kuharibiwa vibaya. (picha na Salmin Said, OMKR)





0 Comments