Na Amina Omari,Tanga.
NAIBU Waziri wa Ofisi ya Makamu wa
Rais,Ummy Mwalimu, amesifu jitihada zinazochukuliwa na taasisi za kibenki
nchini hasa katika kuisaidia jamii kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo
ikiwemo afya na elimu.
Alitoa kauli hiyo wakati akipokea vitanda
saba vyenye thamani ya shilingi milioni
tano kutoka benki ya NMB kwa ajili ya kujifungulia wakina mama wajawazito
katika jiji la Tanga.
Makabidhiano hayo yalifanyika kituo cha afya
Makorora jijini Tanga.
Alisema msaada huo umekuja wakati muafaka
ambao utawaondolea adha waliokuwa wakipata akina mama wakati wa kijifungua.
Aidha aliwataka akima mama wajawazito kuwa na utaraibu wa kuhudhuria vituo vya afya
wakati wa ujauzito ili kujua maendeleo yao
badala ya kuendelea kukaa majumbani.
Awali Meneja wa NMB tawi la Madaraka mkoani Tanga,Juma Mpitimbi, alisema benki hiyo imetoa
vitanda hivyo ili viweze kuhudumia vituo
mbalimbali vya jiji hiulo nambayo ni sera yake
ya kuunga mkono shughuli za kijamii hususani afya.
Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Tanga, Halima
Dendego, alisema msaada huo umekuwa faraja kubwa kwa mama wajawazito.
0 Comments