Na Mwandishi Wetu Pemba.
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Sadiki Iddi Mbarouk,
mkaazi wa limbani Wete amelazwa katika hospitali ya Wete baada ya kupata kipigo
kutoka kwa Wananchi wenye hasira na kumsababishia majaraha na kulazwa katika hospitali
hiyo kwa matibabu.
Kijana huyo anayekisiwa kuwa na umri wa miaka kati ya 25
na30 amefikwa na kadhi hiyo kutoka kwa wananchi wenye hasira akituhumiwa
kukutwa na kuku wanaosadikiwa ni wa wizi.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa shida wakati
akiendelea kupata matibabu katika hospitali ya Wete Sadiki amedai kuwa mkasa
huo umempata jumatatu ya mei 19 mwaka huo majira ya saa nne asubuhi huko utaani
wete.
Na kusema amepigwa na watu wengi tu,wanadai kwamba mimi
nimeiba kuku asubuhi huko utaani na walionipiga wanajuwa wote kwani sikumbuku
kuiba kitu cha mtu, alisema.
Nae Daktari wa zamu katika wodi ya wanaume alimwambia
mwandishi kuwa wamepokea kajeruhi huyu majira ya saa nne na nusu asubuhi.
Alifahamisha kuwa kijana huyo amepata maumivu sehemu za
kichwa ambazo amepigwa na kupasuka na katika sehemu ya mkono wake wa kulia
ukiwa na maumivu yaliosababishwa na jaraha.
Alisema kuwa tayari majeruhi huyo amepatiwa huduma za mwanzo
ikiwa na pamoja na kusonwa sehemu alizoumia na kupigwa picha ya X-RAY, ili
kujuwa hali ya mkono wake.
Ni kweli tumepokea majeruhi mmoja anayefahamika kwa jina la
Sadiki Said Mbarouk, huyu amefikishwa hapa akiwa chini ya ulinzi wa jeshi la
Polisi
Nae Kamanda wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Shekhan Mohammed
Shekhan,amethibitisha kutokea kwa tukio hilo
na kuwataka wananchi kuacha kuchukuasheria mikononi mwao.
Alisema kuwa pamoja na falsafa ya Polisi Jamii kusaidia
kukabiliana na vitendo viovu lakini vyema wananchi wazingatie ukamataji salama
kwa kuhakikisha kwamba wahusika wanafikishwa kwenye vyombo vya dola salama.
Ninawaomba wananchi wazingatie suala la ukamataji salama na
kuacha kujichukulia sheria mikononi mwao bali wawafikishe kwenye vyombo vya
sheria wahalifu wanapowakamata,alisisitiza Kamanda.
0 Comments