6/recent/ticker-posts

Wananchi Wapatiwa Mikopo 1,553b/-

Na Mwandishi Wetu. 
Jumla ya shilingi bilioni 1,553,484,832.zimetolewa mikopo ipatayo 755 kwa wananchi   5,200 wa Unguja na Pemba kwa lengo la kujiimarisha kiuchumi.

Mkurugenzi Idara ya Mikopo Zanzibar Ndg. Suleiman Ali Haji, alisema hayo wakati akizungumza na mwandishi Ofisini kwake Vuga mjini Unguja.

Alisema tangu kuazishwa kwa mfuko huo wa Uwezezeshaji Wananchi Kiuchumi mwaka 1991 na mifuko ya AK na JK mwaka 2009, hadi  kufikia juni 30 mwaka 2013 umewanufaisha  walengwa hao.

Jumla ya walionufaika moja kwa moja na fedha hizo ni watu 5200 kupitia mikopo hiyo 755 iliokwishatolewa, kwani baadhi ya mikopo imetolewa katika vikundi vya watu kuazia watano hadi 25 kupitia SACCOS.

Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa kati ya fedha zote ambazo zimetolewa katika mfuko wa JK na AK,  1,075,264,832. ambazo zimetolewa katika wilaya sita za Unguja, ambazo shilingi 478,220,000 zimetolewa kwawilaya nne za Pemba, hadi kufikia 30 juni 2013.

Akizungumza kwa upande wa marejesho ya mikopo, Mkurugenzi alisema jumla ya shilingi milioni  967,881,671. ni miongoni mwa fedha hizo zilizotolewa, zimeweza kurudishwa tangu mfuko huo ulipoazishwa hadi 30,juni 2013, kama inavyoonekana hapa chini.


Hata hivyo, alikiri kuwa kuna baadhi ya wananchi hadi sasa hawajarejesha mikopo hiyo, jambo ambalo limeenda kinyume na masharti husika ya mikopo hiyo.

Kwa kweli wanaturejesha nyuma wale wote ambao hawakurejesha mikopo na kwamba ile dhana ya baadhi ya watu wanaosema kuwa mikopo hiyo ya Serekali ni lazima iliwe basi wanaenda kinyume na masharti yetu.

Aidha alisema kuwa mikopo hiyo haina riba kwa sasa jambo ambalo pia linawapa fursa zaidi wananchi kuchukua mikopo hiyo.

Sambamba na hilo lakini Mkurugenzi alisema kuwa mikopo hiyo imewalenga sana wanawake 9,870 na wanaume 6,870 wamefaidika namikopo hiyo tangu kuazishwa mwaka 1991.
Tangu kuazishwa huduma ya utoaji mikopo mwaka 1991 jumla ya shilingi bilioni 1,027,289,850. zimetolewa ambapo fedha zilizorejeshwa hadi sasakufikia mwaka jana ni shilingi milioni 967,881,671.

Mifuko imewezeasha wananchi hasa masikini wa mijini na vijiji kujipatia mitaji iliowawezesha kufanya shughuli za kilimo, biashara, uvuvi na ufugaji,hivyo mikopo imekuwa chazo cha upatikanaji wa ajira.

Aliwataka wananchi kuitumia fursa ya mikopo ili kujiendesha kiuchumi na maendeleo yafamilia na taifa kwa ujumla katikampango wa kupunguza umasikini nchini.      


    

Post a Comment

0 Comments