Mwakilishi wa jimbo la Mwanakwerekwe Mhe Shamsi Vuai Nahodha akizungumza na Wajumbe wa Baraza nje ya ukumbi wa mkutano baada ya kuahirisha kikao cha asubuhi baada ya kuchangia Bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar leo asubuhi.
Mwakilishi wa kuteulia Mhe. Shadya akichangia bajeti katika ukumbi wa mkutano wa baraza wakati wa kupitisha bajeti ya SMZ, Mhe wa Uzini Mohammed Raza, akisoma kitabu cha bajeti ili kupata kuchangia katika kikao hichon cha Bajeti kwa Mwaka 2014/2015.
Wajumbe wakifuatilia Bajeti wakati wa kuchangiwa katika ukumbi wa mkutano.
Viongozi wa Serekali wakifuatilia michango ikiwasilisha katika Kikao hicho cha Bajeti
Waandishi wa vyombommbalimbali vya habari Zanzibar wakifuatilia michango ya Wajumbe wa Baraza wakati wakichangia.
Viongozi wakiwa makini kuchukua michango iliowasilishwa na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi katika kipindi cha michango ya kuchangia Bajeti ya Mwaka 2014/2015.
0 Comments